Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Dhana a.k.a Konsepti ya MUDA na MAISHA katika jicho la MTOTO!

>> Thursday, April 16, 2009

Asubuhi,...
....... jioni ni mbali.

Ikifika Jioni,....
.... asubuhi ni mbali.

Mtoto akifunga macho,...
.... viliombele yake hakuna au viko mbali.

Pembeni ya baba,...
.... mama hayuko mbali.

Na swali ukiuliza,...
.... jibu hata la uongo kutoka kwa wazazi au wakubwa ni kweli tupu na haliko mbali.

Na latosheleza udadisi,...
...... kama na pipi haiko mbali.

Pembeni ya kufokewa,...
.... woga na machozi haviko mbali.

Kwa kugombezwa,...
.... kukua na uwoga hakuko mbali.

Kwa kuchapwa na kutukanwa,....
.... kutojiamini hakuko mbali.

Kwa kupendwa,...
... amani , upendo na furaha havina umbali.



Dunia haitishi kama amani iko nyumbani.

Na dunia yote ni wazazi, ndugu, jamaa na marafiki hata wale buriani.

Labda mpaka mtoto aambiwe na kutishwa , asiyemjua ampitie mbali.




Na kama wewe ni Mzee,....
.... wakumbuka bado kuna mtoto ndani yako kwa ndani?


Kama ni mtoto yatima,....
.... labda ni vigumu kujua wapi na nini nyumbani.

Na yatima utajifunza ya utu uzima,...
... wakati kuwa mzima ni shughuli ya kuotea mbali.


Na ukimgundua mtoto ndani yako, ...
.... kesho haitishi hata kama haiko mbali.

Ingawa kama mtoto ndani yako katishiwa kuhusu ya mende,...
... bado kutishika na mende hakutakuwa mbali.

Na katika maisha yategemea ni mtoto gani wamkuza,...
.... katika maisha haya ujue unaishi maisha gani na ufike mbali.

Swali:
  • Lakini si bado siku yako utotoni ilikuwa ina masaa ishirini na nne kama siku yako ukubwani?


NIMEACHA na ni moja tu ya WAZO mkuu, usitishike!

Tutulie tena kwa kwenda Haiti kukutana na Wyclef Jean ft T Vice + Buju wadai- Party by the sea


Au tu ST Germain wajazzfai tena katika - Rose Rouge

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP