Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kama ungekuwa na ukubwa wa SISIMIZI na unajaribu kuelewa ukubwa wa MTU!

>> Thursday, April 09, 2009

Inawezekana kwa SISIMIZI mtu haonekani na maisha ya mtu kwa sisimizi ni MILELE.

Na ukipiga teke jiwe alilopo sisimizi lika vuka mfereji na sisimizi , kwa SISIMIZI ataona MUUJIZA umetokea kama tu ukidondosha kibonge cha sukari na kumletea SISIMIZI kitoweo pale asipotarajia.



Swali:

  • Ushawahi kujiuliza kuwa labda MUNGU wa BINADAMU hasa yule wamuaminiye wawamuaminio MUNGU ASIYEONEKANA , haonekani kwa binadamu kutokana na UKUBWA TU kama SISIMIZI asivyomuona MTU?
  • Ushawahi kustukia kuwa hata utumbo wako ni ulimwengu wa baadhi ya bacteria ambao wanaumbwa na kufa kabla yako MUMO KWA MUMO wakiishi kwa manufaa yako ya kulainisha chakula na kukusaidia kukutengenezea kinyesi bomba?
Na ukimkanyaga sisimizi ni kiama kwa sisimizi!:-(

Nimeacha!
Na ni moja ya wazo tu kumbuka!

Badili Mudi kwa kusikiliza En Vogue wadai -Dont let GO...


Au tu Michael Jackson aseme -WORKING DAY and NIGHT

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP