Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kumpenda MPENZI tu labda HAITOSHI ndio maana sio wote kwa kitendo cha kupewa PENZI wanapata MAPENZI!

>> Monday, April 13, 2009

Inasemekana wanawake hawasikii kama wanaume na wanaume wenye sikio zuri la wanakike , ni wasenge!:-(

Na labda ni kweli kama wewe unamtunza MPENZI au una penzi basi wewe ni bingwa wa michezo ya akili.

Na,...
...hata ukilivutia punzi penzi unaweza kuambulia mwili na sio penzi ndani ya michezo ya akili ya apendaye na apendwaye yenye mwili.


Na usipoangalia huu ndio wakati unaweza kufikiri unapatapenzi, kumbe mtu kafikia hatua ya kuwa anachokupa ni kikojoleo na kiungo cha kutemea mate na sio tena kiungo cha penzi na busu katika penzi.

Na huhitaji kuvutia punzi au kututumua misuli kujua umeachana na mpenzi, kwani kitendo chakumuacha mtu hakihitaji nguvu wala akili:

Siku ya kumuacha mpenzi kimapenzi utajua tu umemuacha hata kama hutamuambia na utaendelea kuendelea kuishi naye katika hii michezo ya AKILI ya PENZI na kutobadili uliyokuwa unafanya wakati unapenzi! Na kikwapa chake utakistukia.


Na katika michezo ya akili, anayechunwa buzi anaweza akawa anajua anachunwa buzi na hiyo ndio kete yake katika michezo ya akili ya PENZI na anajisikia vizuri angalau unaona anafaa angalau kwa kuchunwa buzi, na ni PENZI!

Na pamoja na yote bado nivigumu kuwa na uhakika umepata mpenzi hasa katika dunia hii ambayo mwanamke na mwanaume wanatokea sayari tofauti na swali moja linaweza likawa linataka jibu tofauti na swali hasa kama ni mwanamke anauliza na sio katika PENZI.

Na bado,..
..... katika MICHEZO YA AKILI hata kulia IMO , ingawa wakati unalia ili mpenzi AKUONEE HURUMA, unaweza ukawa unalia kirahisi kwa kufikiria lile shamba la mihogo ambalo mkiachana ndio nalo limetoka hivyo:-(


NIMEACHA!
Nawaza tu kumbuka hilo MKUBWA!

Swali:

  • Unauhakika gani kuwa wapenzi uwaonao wanapendana na sio mmoja ndio ampendaye mwingine?

Namuacha Erykah Badu adai - Didnt cha know


Au tu Arrested Development waseme- Mr Wendal

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:32 pm  

Mmh, Simon Hapo kakangu ipo kazi tena kazi kwelikweli:-)

Simon Kitururu 4:03 pm  

@Yasinta: Kazi kwelikweli!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP