Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Bado ni KWELI dunia imeharibiwa ZAIDI na WASIOLEWA waliowengi katika JAMII!

>> Sunday, April 05, 2009

Kama asiyelewa ndiye haelewi mlevi kuna uwezekano asiyelewa haelewi hata yake aaminio hayana ULEVI!

KAMA unalewa,....
....labda usiamini wasiolewa kwa kuwa kuna MTAZAMO unajua hawana.

Na jihami na asiyelewa anayekojoa pembeni ya barabara !:-(

Na,....
.... ukimfuatilia ASIYELEWA anaweza kukusimulia hata CHAI wakati hana jibu ukimuuliza ni nini LADHA ya chai.


Swali:

  • Unajua ladha ya chai ni nini ingawa labda hata huwezi kutungia shairi chai na HUJALEWA?

Na ni kweli,...
... WASIOLEWA ndio MAJORITI ya waliofikia UTAALAMU wa kujiua wa KITALIBANI au kwa sababu za kuamini bila kuamini kuwa wamelewa na wasivyoita ULEVI, wanaamini mpaka hata yale YASIYOAMINIKA kama yale waitayo DINI.
Swali:
  • SI unakumbuka kuna walewao NYUMBANI na kunajisi ingawa alalamikiwaye kulewa ni arahisishaye kujulikana mlevi kwa kunywea pombe baa?
  • Unakumbuka washindwao kutatua matatizo ya nchi karibu wote hawajalewa na wafanyacho hakieleweki hata na haohao wasiolewa?

Kumbuka sisifii ulevi hapa na bado POMBE SI CHAI!


DUH!
Ngojea tu AWILO LOMGOMBA azungumzie-COUPE BIBAMBA....

AU ngojea turudi tena JAPANI kukutana na HIKARU UTADA aongelee kitu katika wimbo uitwao - Boku wa KUMA

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 8:45 am  

Kaka Kitururu,

ahsante kwa simulizi za mlevi.
nahisi kama na wewe ni mlevi! kwani khuweze kuandika habari za ulevi kama hujui ladha ya pombe.

Masangu Matondo Nzuzullima 10:07 am  

Ngoja kwanza nikajikumbushe falsafa za walevi hapa:
http://matondo.blogspot.com/2009/01/falsafa-ya-mlevi-1_30.html

Nitarudi baadaye!

Yasinta Ngonyani 1:42 pm  

Koero, hata mie nahisi hivyo hivyo kuwa Kaka Simon popmbe/ulanzi hazikupiti-:)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP