Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ASIYEAMINI zaidi ya YA UBINADAMU kapungukiwa, na AAMINIYE MUNGU au hata ya SHETANI anaishi maisha ya kujifunza IMANI na kutafuta UKWELI mpaka AFE!

>> Monday, April 13, 2009

YAKIBINADAMU tu hayatoshi,...

.... YA MUNGU yanachanganya.....
.... na ya SHETANI hayakawii kuisha UTAMU.



Binadamu katika kujazia mapungufu, .....
..... hujaribu kuongezea ya MUNGU, Miungu au hata ya SHETANI
na ukweli katika imani kirahisi tu unaweza kujikuta unapitia

  • Kutokuwa na IMANI,
  • Kujifunza Imani,
  • KUAMINI ,
  • kupungua imani,
  • kuacha kuendekeza imani na hata mwisho kuanza KUAMINI TENA!
Yote huwezekana ndani ya maisha ya binadamu!

Na ukifa wakati tunaamini unaamini tunachoamini kama vile MUNGU, katika mazishi yako tutadai umeenda MBINGUNI!

Na tukiwa na wasiwasi na imani yako wakati unatutoka, BADO tunaweza tusikiri hadharani kwa kusema tunauhakika unakwenda kwa SHETANI ingawa kwa kimoyo wazo hilo lipo.

Swali:
  • AU?


Kuna sababu karibu kila jamii DUNIANI kuna kitu inaamini ambacho kinaoanishwa na kuwa na uwezo kuliko binadamu hata kama hicho kitu ni binadamu kama walivyokuwa MAFARAO Misri.

Na atafutaye jawabu na faraja KATIKA IMANI ashawahi kukwama kibinadamu!

Na kama ushawahi kukwama kibinadamu labda ushaanza kuwa na BUSARA.

Swali:
  • AU?
  • Bado hushangazwi kwa wasiojua vizuri hata dini zao walivyonauhakika na kasoro za dini za wenzao?


NAWAZA TU MKUU hapa MAWAZONI usitishike!
Tutulie na Black Uhuru waulize- What is life

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:06 pm  

kuwaza lakini angalia usiwaze sana:-(

Simon Kitururu 4:04 pm  

@Yasinta: Kweli kabisa!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP