KATIKA kutostukia nyege za UPUUZI mpaka baadaye kidogo baada ya kumalizia KUFANYA UPUUZI!
>> Thursday, April 09, 2009
Wapuuzi wengi hawana nia ya kufanya UPUUZI, nikatika kumalizia kitendo wanastukia au kustuliwa kilikuwa ni kitendo cha kipuuzi!:-(
Na,...
... upuuzi NISHAI!
Upuuzi wa LEO unaweza usiustukie mpaka MWAKA KESHO,
....Na...
Isingekuwa hivyo waheshimiwa wengi wasingeumia roho baada ya kufumaniwa baadaye kidogo baada ya kuwa WAHESHIMIWA kuwa yaliyowapa sifa JANA labda hata uheshimiwa, karibu yote LEO ni UPUUZI.Na labda,...
.... wengi wasiofanya UPUUZI hawafanyi upuuzi kwa kuwa hawajitahidi kutofanya upuuzi bali wamebobea TU kujaribu kuishi tu LEO maisha yao kama kawaida , kama ilivyokuwa JUZI.
Na ,....
... wale wajitahidio kutoonyesha upuuzi wanasifa labda hata za kujisifia,...
.... ingawa....
ukiwaangalia wengi wao wamenunia shughuli nzima leo usijekushuhudia wakifanya upuuzi leo ingawa kama kawaida ya ubinadamu wapo WATAZAMAJI na WASIKILIZAO wasubirio mpaka kesho kutafsiri ya leo.Swali:
- Unauhakika mheshimiwa ahitajiye kuheshimiwa sio mpuuzi kwa hilo?
- Unauhakika hujawahi kubadili mawazo kuhusu ulichodhani ni upuuzi na leo unadhani ni njia ya kwenda mbinguni?
Ni kweli kabisa,...
... wengi wakati wanahangaikia kukwepa upuuzi hufanya UPUUZI kwa kuwa vigezo vyao vya kwanini sio upuuzi ndio KIINI, MISINGI na tako la UPUUZI!
Sikubishii lakini ukinibishia!
Naacha UPUUZI kama unauhakika nilichoandika ni upuuzi!:-(
Swali:
- Unauhakika wakati unataka kumbishia ambaye haelewi utakachokufanya sio UPUUZI kama hujajaribu kumelimisha?
Kumbuka HATUKUONI na USIJIHAMI!:-(
siKU Njema!
Hebu tumsikilize AL PACINO katika sinema SCARFACE....atoe -BAD GUY SPEECH (jihadhari lugha chafu!)
Au tena Les Wanyika wamuongelee -Paulina
Au tu twende Ivory Coast tukutane na Joelle C - MAN DINKA
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kaka nimepita hapa kusoma upuuzi,
@Kaluse: Asante kwa kunitembelea!Dozi ya upuuzi ni muhimu katika maisha haya yasiotaka upuuzi!
Kazi ipo katika jinsi ya kubalansi upuuzi na sio upuuzi katika kuona picha kubwa katika maisha!
Post a Comment