Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Jinsi BLOGU na INTERNET ziendeleavyo kukosesha UHURU WA KUBLOGU na kuwa huru kwenye INTERNET !

>> Monday, April 06, 2009

INASEMEKANA kama unataka UHURU wakutaka kuongea utakayo na kuyaweka wazi bila vipingamizi vya mhariri, UNAWEZA kuanzisha BLOGU au kuweka tu mawazo yako kwenye internet!

Lakini kumbuka,...
...hata UHURU WA KUSOMA unawezakusababisha USISOME!

Tatizo ni,...
..... unaweza kustukia jinsi gani usivyo huru kwa kujikuta hauko huru HATA kama uko peke yako kwenye BLOGU na internet!

Na usipoangalia LABDA umeshajibatiza mpaka jina jingine kwenye BLOGU au INTERNET kwa UHURU kama wewe hutumii jina LILE maarufu la ANONYMOUS ,hasa PALE ukitaka kujaribu kwa mara nyingine kuwa HURU angalau kutoa dukuduku lako kwa uhuru wewe UDAIYE UKO HURU.:-(

NA,....
..... baada ya miaka kibao ya HABARI kuwa ni BIDHAA HADIMU ambayo watu wachache ndio wawasimuliao wengine kuwa leo HABARI ni nini, sasa kumezaliwa Blogu, Twitter ,nk. na YOUTUBE inashindana na TELEVISHENI ingwa ni wachache watumiao hizi tekinolojia WAKO HURU kukuambia wanachofikiria kama wewe ni mlengwa na wanadhani hawatanufaika kwa wewe kujua wanavyo kufikiria.

Swali:

  • Unauhakika katika KUNDI hujali na kuthamini zaidi kusikilizwa na BAADHI tu ya watu fulani katika kundi la watu ukipewa uhuru?
  • Unakumbuka kuwa kwa udhaniaye ana akili huwa unaruka kutilia maanani YALE yake ya kijinga kwa uhuru?
NA,....
.....Kumbuka wote tunaongea ingawa UNAMSIKILIZA zaidi kwa HIARI na UHURU aongeaye upendayo KUSIKILIZA!:-(


  • Kabla sijaongelea JELA ya UHURU , .....

....KUMBUKA inasemekana,...
Kwa uhuru ni rahisi kukimbilia mambo rahisi kwa BINADAMU mwenye silika ya UVIVU na hamu ya kurahisisha!

Na binadamu unaweza kumgawanya katika makundi mengi ingawa kirahisi unaweza kumgawa katika makundi kwa kustukia kuwa ni Mwanamke au Mwanamme na je ana UMRI GANI hasa kama hamu yako ni KUSIKILIZWA. Lakini pamoja na kumjua utakaye kumuongelesha, bado unaweza kukosa uhuru wa kusema UNACHOFIKIRIA.



Na,...
.....hata kwa kutumia KIGEZO CHA KIJINSIA TU, inajulikana binadamu anavutiwa na kupitiwa mawazoni na mambo kadhaa yajirudiayo kila siku kwa kigezo hata hicho cha kuwa ni mwanamke au mwanaume.

Na kama unataka kumdaka umtakaye akusome au UMTAKAYE TU, jaribu kumjua umlengaye yuko katika kundi gani, hata kama vigezo vyenyewe ni vya kumsaidia mlengwa aliyeko kwenye kundi kuendelea kubakia katika kundi zaidi ya kuondoka katika kundi, kwa kuneemesha dalili za UDHAIFU wa mlengwa utakaye akusikilize kwa KUTOKUWA HURU HATA KUMSHAURI kama amepotea ili asikuone wewe MBAYA kitu ambacho kinakukosesha UHURU.


Lakini bado ;.....
  • Kama unataka kusikilizwa na MCHAMUNGU ongelea DINI au MUNGU.
  • Kama unataka ueleweke na mvivu wa kufikiria lakini anapenda korosho na miwa, rahisisha topiki kwa kumuonyesha picha ya korosho kuliko riwaya ya korosho na mkatie vipandevipande MUWA ili asione uvivu kula miwa.
  • Kama ni mwanamume wa umri fulani, ni rahisi kujua kuwa hata bila ya kumuuliza ni mara kadhaa anafikiria mwanamke na yahusianayo na uke na kirahisi atakuwa rafikiyo ukiongelea matiti na uke.
  • Kama unamjua aliyezoea kulalamika , jifanye unaelewa alalamikacho halafu na wewe KILALAMIKIE.
  • Kama anapenda UDAKU rahisisha ujumbe kwa kuwa anaweza kukubishia wewePROFESA WA SWALA kwa vigezo alivyosimuliwa na MWANA SHULE YA VIDUDU.
..... na kwa kufanya utarajiwacho kufanya ikiwa ni katika kumlenga mlengwa ili akusikilize, bado UNAJIPUNGUZIA UHURU.




  • Kabla sijagusa KIINI cha KIDONDA, ngojea nianze kwa kusema;.......

Kumbuka tena wote tunaongea ingawa UNAMSIKILIZA zaidi kwa HIARI na UHURU aongeaye upendayo KUSIKILIZA!:-(

Kumbuka kila utembeapo unakutana na MAMIA kama sio MAELFU ingawa unamuona na kumkumbuka uliyemuona katika mamia KWA UHURU ni yule ULIYEMLENGA KUTOKANA NA AKUGUSAVYO ingawa aliyepembeni yake labda ndiye mwenye jibu la TATIZO LAKO hata lile la UKAME!

Kumbuka ukiwa huru, ...
.... uhuru hauna maana, na neno UHURU halitakuwa katika MSAMIATI WAKO.



Na,...
..... usipoangalia unaweza kuendelea kudhani watumiao hizi teknolojia mpya za KUHABARISHANA kwa uhuru kuwa wako HURU kwa kuwa wanasema WEWE USICHOTHUBUTU KUKIONGELEA HADHARANI.!:-(

Na labda,...
..... waandikao au wawekao video zao kwenye neti, wanatumia tu zaidi UHURU WAO WAKUTOKUWA HURU!

Swali:
  • Kwani ni tatizo kutotumia uhuru kama uko HURU?
  • Uko huru kwenye INTERNET kama usivyo huru mtaani?

NIMEACHA!


Pumzika kwa hizi Motivational quotes..

na Bill Withers adai tena -Aint no sunshine when she is gone


Au tu SONIQUE adai -It feels so good!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP