Kuna MAMBO huhitaji KUYAELEWA!:-(
>> Friday, April 17, 2009
Ndani ya mambo MILIONI ndani ya siku,....
.... KUBALI kushindwa yote KUELEWA ili uishi kwa furaha.
KUELEWA sana ni siri ya KUTOELEWA SANA,...
....hasa katika pande na SURA MIA za KITU KIMOJA wakati mmoja.
LAKINI elewa KIELEWEKACHO,...
... kwa kuwa ukijifanya HUELEWI UELEWACHO,...
KUNA JAMBO UNAELEWA!:-(
Swali
- AU?
Ngojea Kool and THE Gang waseme -Hi De Hi Hi De Ho
Au tu YellowMAN adai -AFRICAN CHRISTMASS
5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Mi sijaelewa:-(
kaka Kitururu,
Ni siku nyingi sijapita hapa kibarazani kwako....
kusoma vibweka na vifikirishi vyako...
bnaona umepunguza ukali wa maneno...
Hongera
Simon,
Umenena yaliyo kweli. KUna mambo mengi ukiyajua, ndio unakuwa mwanzo wa mwisho wako.
Ndio maana kuna rafiki yangu mmoja alikuwa akitania siku moja kwamba akili ya mwanadamu ni vyema ikawa gizani (tuwe wajinga) ili tuishi kwa amani. Tuchukuliane na watu. Kwa sababu hatuoni tunachopaswa kuona.
Akili hiyo hiyo ikifunguliwa kwa kupewa elimu ya kweli kweli, ndipo mgogoro unapoanzia. Kila kitu kuhoji. Kwa kuona wasichokiona wengine basi unakuta unakosana na watu.
Huenda ni kweli. Bila shaka.
Lakini je, hasara ya kuyajua mambo inaweza kufanana na hasara ya ujinga?
@Yasinta: :-(
@Dada Koero: Asante!
@Bwaya: Halafu inatisha!Bado mimi ninafeva kujua lakini!:-(
Post a Comment