Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKO HURU?

>> Thursday, April 02, 2009

LABDA,...
.... huwezi kuwa huru DUNIANI kama nia yako ni kwenda MBINGUNI!



Na labda,...
... walio huru ni wale wafanyao DHAMBI kwa uhuru wakijua ni DHAMBI!

Na,..
... huwezi kuwa HURU NA YAKO kama nia ni kutunzia mpaka NDUGU, JAMII na MUNGU heshima!


Na labda,...
... kutunza kwako HESHIMA ni aina ya UTUMWA!:-(


  • .......utumwa wa kujaribu KUTOVUNJA heshima!
  • .......utumwa wa KUHAKIKISHA unaheshimiwa!
  • .........utumwa wa KUTAKA uheshimike!
Na labda,...
... kutafuta elimu ni kukiri HAUKO huru!:-(
  • HAUKO HURU na ujinga!
  • HAUKO tu HURU!

Na labda,...
.... kuelimika ni KUKIRI kunakitu HUJUI na kwa kujua HILO unaongeza UHURU wa kujaribu KUJUA.

LAKINI pamoja na yote labda ,...
..... haiwezekani KUJUA , na huwa tunajaribu tu kujua MAZINGIRA HAYA yakiruhusu ya mazingira haya, ingawa MAZINGIRA YAKIBADILIKA ujuayo ndio USHAHIDI ukutambulishao kuwa HUJUI.


Swali:

  • Uko huru?
  • Unakumbuka kuna starehe pia ya kukosa uhuru kama huhitaji kuwa huru?
Na,....
.... kama kuna kitu UNALAZIMIKA hata kama ni kulazimika kuamka, LABDA hauko HURU!:-(


Kumbuka ninawaza tu!
ALHAMISI NJEMA!


Pumzika kidogo na Idi Amini mtu wa famili, kama una muda.


Au twende tu REUNION kukutana na Granmoun Lele aseme - Soleye

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:39 am  

Simon kama una amini kuwa upo huru basi upo huru:-)

Anonymous 6:15 pm  

Mkuu
nimekupata kuhusu jumuwata.


amani mkuu
rasta hapa.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP