Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Uwezekano wa MJINGA KIJANA kuzeeka MJINGA!

>> Tuesday, April 14, 2009

Hakuna fomwula za kuacha au kujifunza ,....
......kwa kuwa tu jambo UMELIPITIA!:-(

Unaweza kuzeeka na UJINGA ingawa tokea ujanani ....
.....Ujinga UMEPITIA.

Kwa kupitia kitu unaweza ukachanganyikiwa na kuchanganyishwa zaidi na ...
......usijifunze wala kujua ingawa yote UMEPITIA.

Na kwa kuuzoea ujinga , ...
.... unaweza kukomaa kwa ujinga usiuone tena ujinga na yote ni kwa sababu UMEUPITIA.


Kwa kuzeekea shughuli ,...
... unaweza kuzeeka na shughuli tu, na usijue shughuli UNAYOIPITIA.

Swali:
  • Unafikiri ndoa ihusishayo mabikira wawili ambao shughuli bado hawajapitia sio bora kuliko ya wale waliokomazwa na shughuli na advencha za hughuli wameacha kupitia?

  • Kwani hujawahi kukutana na Mzee MJINGA?



NA bado ni kweli,...
..... kila mtu anachakukufundisha kwa kuwa karibu kila mtu kuna kitu sio MJINGA!
Na,...
.... mjinga anaweza kukufunza jinsi ya kuwa mjinga madhubuti!
Swali:
  • AU?

Ni moja ya wazo tu katika UjingaBUSARA na USITISHIKE!

Siku njema!

Ngojea Sanchez aseme -Baby can I hold U tonight


Au tu Buju Banton na Wayne Wonder wadai-I dont know why

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:22 pm  

kazi kweli kweli:-(

Simon Kitururu 1:58 pm  

@Yasinta: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP