Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

SI BADO unajua HADITHI wasimuliwazo WATOTO na WAKUBWA, huwa ALIYETUNGA ni MKUBWA?

>> Thursday, April 23, 2009

Watoto ni wabunifu kuliko wakubwa wa HADITHI na kama unabisha wavizie wakicheza usikie wanavyosimuliana hadithi walizobuni wakati wanaendelea kuzibuni.

Kikubwa ni,...
... hata mtoto ukimuacha acheze mwenyewe, kama aliwahi kuona gari anaweza kugeuza ndala liwe gari na pia akajisimulia mwenyewe STORI kuhusu kuwa hilo gari aina ya NOLINOLI a.k.a ZIMAMOTO au ze AMBULANSI na jinsi lilivyookoa mtu na mende!

Swali:

  • Hivi hapa sijadanganya kweli kuwa watoto Wakibongo waliowengi wanajua kuna gari la wagonjwa na zimamoto a.k.a NOLINOLI?

Tuendelee.....

Ukikutana na MKUBWA anamsimulia mtoto hadithi iliyotungwa na MTOTO basi huyo mkubwa SPESHO!

Tatizo ni,...
.... stori a.k.a hadithi za wakubwa ndio zisakiziwazo watoto kwa kigezo cha kuwa zinamafunzo.

Na kama wakubwa wangekuwa wanajifunza na wanamafunzo , akina Yesu, Mohamedi, Gandhi, Babu Mrinde, na hata BULICHEKA na ABUNUWASI kuna mambo wangekuwa wamemaliza enzi hizo kufunza waliotutangulia wenye uume na uke, na siye wengine hata wasiwasi wa UKIMWI kama tu KASWENDE achilia mbali KUFA NA NJAA , tungekuwa hatuna kama jinsi tusivyokuwa na wasiwasi na matumizi ya choo cha shimo.


Na naamini HISTORIA haitufundishi kitu kutokana na STORI za wakubwa kufundishwa watoto , WATOTO wenye stori orijino.

Stori za wakubwa ukiziangalia vizuri , ni za Kiyesuyesu au za TISHA TOTO zisababishazo watoto HATA WAKIKUA wanakuwa WATOTO WAKUBWA halafu wengine ndio hawa tunawaita VIONGOZI WAHESHIMIWA WAKUBWA waendeleao kuongoza na KUTULEA kwa staili za TISHA TOTO!

Sikatai umuhimu wa uzoefu!
Sikatai ukisimulia uzoefu wako, na labda ndio maana wengine tumejifunza mpaka katerero kutokana na stori na sio kupiga chabo.

Lakini ukitazama , utastukia kuwa ni hadithi za wakubwa zinazopelekwa kwa watoto na kuendeleza sanaa za kutaka kutafsiri kwa watoto kuwa kwa kuwa wewe sio kama mimi kwa kuwa mimi na kifafa, basi unikwepe nikijamba usijepata kifafa , wakati kifafa inajulikana hakiambukizwi kwa ushuzi.

Na stori hizi a.k.a hadithi hizi ndio hizo zinasababisha toto likikuwa lifikirie sijui likubake au kukupiga konzi kama sio kukubagua kwa sababu wewe:
  • Zeruzeru
  • Muarabu,
  • Muhindi
  • Chotara
  • Jeusiiiii
  • Pua kama nundu
  • Sangara wamo
  • Titi ndimu na chuchu mwiba
  • Meno kama ngiri
  • Ustadh
  • Mlokole
  • BAYAAAA!
  • ZURIIII!
  • Muafrika
  • Muislamu
  • Mkristo
  • nakadhalika tatu na nusu.
Swali:
  • AU?
Na,...
...KUBWA ZIMA sikiliza watoto wakisimuliana hadithi orijino ugundue kitu au hata ugundue HADITHI NI NINI.

Na kama simulizi lako ni la yaliyotokea kweli, SIMULIA ingawa nayo inaweza kuwa ni HADITHI ila isiyotungwa. Na simulia kama unafikiri ni kweli ni lazima kila stori huwa inabidi isimuliwe.

Swali:
  • AU?
  • Si unakumbuka kuwa si kila hadithi hutungwa?
  • Unafikiri ni kwanini kuna unavyoacha kutusimulia na kwa vigezo gani kuna utusimuliavyo?

Nimeacha na ni moja ya wazo tu !
SAMAHANI!

Tulia na stori ya Sam na Esther (WARNING! Ni ya HUZUNI!)

Au mpate tu Innocent Galinoma asimulie kuhusu ya- RAIN

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 9:47 pm  

Mi najua wote ni watu au:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP