Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati wewe UNASHINDANA na WEWE!

>> Friday, September 04, 2009

Kama unashindana na wewe labda hakuna ashindaye,....

.... na ukidhania unashinda labda huo ni ushindi wa mwisho!:-(


Na kama KATIKA YAKO mashindano, DHAMIRA inakugawa weye,....
... dhamira ikushawishiyo UDOKOE MBOGA ikishindwa na dhamira ikukatazayo KUDOKOA MBOGA.... au tu ikiwa ni mshindi wa pili, kumbuka bado DHAMIRA ILIYOKUSHAWISHI UFANYE bado imeshinda hata kama ITADAIWA ni DHAMIRA mshindi wa mwisho!:-(

Kumbuka mshindi wa mwisho ni mshindi hata kama huitwa wa mwisho NA bila wa mwisho adhaniaye ana USHINDI wa KWANZA NI NYOKO na ukweli labda mkitolewa BARUTI kutokea mbele, yeye YUKO mwisho.

Na tukiwa wawili na ukanishinda, kumbuka NINA haki za kushangilia ushindi wangu wa pili hata ukiitwa wa mwisho,KAMA unamaana kwangu ZINIPELEKAZO JUU hata kama NAENDA JUU huku niko hukohuko MWISHO.

Swali:

  • Unakumbuka mgambo wakitokea waanzao kupigwa virungu sio waliokuwa mwisho?
  • Hivi mtu akishinda na kuwa wa kwanza si maana yake inabidi aanze upya kwa kuwa kwa kifupi mchezo inabidi uanze upya na ushindi uliopita ushageuka NYOKO?
  • Unakumbuka mashindano ya binadamu yaliyo mengi KAMA SIO YOTE yako KICHWANI MWA Binadamu na wala HAYAKO KWA mtu kushindana na mtu au vifaranga wengine, kwa hiyo kwa kifupi ina maana ukishinda maana yake bado na kushindwa kumekung'ang'ani kipengele?

  • Unafikiri mshindi wa mwisho hajashinda?

  • Unakumbuka inasemekana mshindi wa mwisho ndio hujifunza kuliko mshindi wa kwanza?


NI wazo tu KIJEBA!

Hebu twende Tanzania Ras Nas alete kitu -River Nile...




Au tu tubakie hapa hapa Tanzania Jhikoman azungumzie-Mapenzi

Read more...

Tanzanian Bloggers Summit!










Je wewe ni mwanablogu (Blogger) au mdau wa habari na mawasiliano kwa umma kwa kutumia mtandao? Kama jibu ni ndio, tafadhali unaombwa kujiorodhesha kwa ajili ya maandalizi ya Kongamano Maalumu la Kitaifa kwa ajili Wanablogu (Bloggers) na wadau wa habari na mawasiliano wa Tanzania (Tanzanians Bloggers Summit) linalotarajiwa kufanyika Desemba mwaka huu jijini Dar-es-salaam,Tanzania.

Dhumuni la kongamano hili ni Kuelimishana, Kufahamiana, Kuamsha Utambuzi Rasmi Kuhusu Tekinolojia ya Blogu na Mawasiliano ya Umma kwa Kutumia Mitandao, Kusaidia Utambuzi Rasmi juu ya mchango wa blogu nchini Tanzania kama chombo muhimu cha habari na mawasiliano, Kuelimishana jinsi gani blogu zinaweza kutumika katika kuleta maendeleo katika nyanja za kijamii, kisiasa na kiuchumi, kuburudisha, kukuza utamaduni nk.

Wataalamu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wataalikwa kutoa mada na mafunzo mbalimbali kuhusiana na tekinolojia ya kublogu, zana nyinginezo za mawasiliano mtandaoni kama vile mitandao jamii(social networking), online forums nk.Kutakuwa na vipindi vya maswali na majibu.

Ili kufanikisha maandalizi ya Kongamano hili la kihistoria, kujiorodhesha kwako ni muhimu sana. Muda wa kujiodhoresha ni kuanzia tarehe 12/8/2009 (Jumatano) mpaka 12/9/2009 (Jumamosi) tu.

Kinachohitajika ili kujiandikisha ni :

Jina Lako, Anuani yako ya barua pepe (E-mail), Mahali Ulipo au unapoishi (Nchi,mji nk),Namba ya Simu (sio lazima) na Anuani au URL(Universal Resource Locator) ya blogu yako (mfano www.kongamano.blogspot.com/wordpress.com/.com/typepad nk). Vyeti vya Ushiriki vitatolewa kulingana na habari utakazoziorodhesha hapa.

Unaweza kujiorodhesha kwa kutuma ombi lako kwa barua pepe kwenda; summit@bongocelebrity.com.

Zingatia tarehe za kujiandikisha.

Ni mwezi mmoja tu! Asante kwa ushirikiano. UMOJA NI NGUVU!

Read more...

Wakati UMPENDAYE kimapenzi anakuita RAFIKI TU na anapenda kukusimulia ya LIMTU JINGINE alipalo PENZI!

>> Thursday, September 03, 2009

Atakusimulia MPAKA ya wake MPENZI!
Na kwa kumpenda wavumilia ili utunze angalau wake URAFIKI,.....

....na kinafiki inabidi UCHEKELEE,...
...na kwa watazamao unaonekana UNACHEKELEA!:-(

Wakati unaagananaye unamkumbatia KIMAPENZI!
Na yeye kwa kukuaga juu ya mkumbatio eti anakupiga na busu adailo ni la tu KIRAFIKI,....
.....anakukonyeza PIA ili UCHEKELEE,...
... na kwa mtazamo wake UNACHEKELEA!:-(


Na unajikuta bila kupanga umekuwa mnafiki kwa kuficha PENZI!
Na ukimuona akiwa na wake mpenzi angekuangalia angejua wakati huo we we ni MNAFIKI na si RAFIKI,...
... ..na sasa inafikia vikuumizavyo moyo inabidi UVICHEKELEE,...
.... na vinakuliza mpaka roho wakati dunia nzima inadhani UNAVICHEKELEA!

KWA KUMUELEZA MPENZI UMEJIFIA yadaiwa utaharibu URAFIKI na sasa wafa na PENZI!
Na kama si mnafiki labda bado huo ufanyao sio URAFIKI,...

...na unajua ni ukichaa KURUHUSU vikulizavyo kukufanya UVICHEKELEE,...
.....Na BADO ni UNAFIKI kufanya wakulizao wadhani UNAWACHEKELEA!:-(

Kihitimisho ni kwamba labda umpendaye anakosa yote yako ya urafiki na ya PENZI
Wewe wabakia wajijua ni MNAFIKI na si RAFIKI,.....
....na NI UAMUZI WAKO na kama waona inalipa umia tu kama maumivu yanakufanya UCHEKELEE,....
..... ingawa labda UTAKAYE LAKE PENZI ukweli huo anaujua na kwa KUJIFANYA HAJUI ni staili YAKE tu yakukunyima huku akiwa bafuni kuisafisha ANACHEKELEA!:-(

Duh nimeacha na kumbuka hili NI WAZO TU NJOLINJO na wala sikuongelei wewe MHESHIMIWA!:-(

Swali:
  • Unauhakika urafiki ni nini?
  • Si inasemekana Urafiki ni aina la penzi tu?
  • Kwani hujawahi kusikia waliopendana kimapenzi wadumupo HATA katika ndoa kiwafanyacho wadumu ni mazoea na labda hata hawafanyi yaliowahi kuwapeleka mpaka migombani enzi zile hayo mapenzi?

Sawa mkuu ngojea tubadili hali ya hewa kwa kwenda tena South Africa kwa Vyonne Chaka Chaka aongelee-Stimela



Au tubaki tu hapa hapa South Africa Athur Mafokate arudie tena-Oyi Oyi

Read more...

MUDA fulani KATIKATI ya maisha ni NYOKO hata kwa wa LEO ajisikiaye ni MTOTO MZURI!:-(

[Tahadhari: Hadithi hii labda haimuhusu msichana ingawa imeandikwa kwa kuegemea mrengo wa kiume.:-(]



Kila MTU anamuda wake wa NYOKO katika MAISHA,...
... .. hasa pale UTOTO UZURI inapobidi uishe mbele za watu....
...na ukubwa kuingia na unajua ukubwa NI MWANAHARAMU!:-(


Na kuna MUDA kuna PRESHA kwenye MAISHA,...
..... na ndizo zigeuzazo waliojulikana watoto wazuri na watu....
....kuwa hawahawa uwashangaao kwa wafanyayo UYASIKIAYO na KUSHUHUDIA yageuzayo dunia JEHANAMU.


Na labda ipo siku utampa au utapewa mimba na HILO ni moja katika MAISHA,...
...na watoto wazuri utakaototoa[ Hapa nazungumza kwa mrengo na mtazamo kuwa labda bado hujatotoleshwa au kutotolesha:-(] wasio hata na DOSARI moja ya NYOKO wapendwao na watu...
...kwa DUNIA ilivyo sasa hivi usishangae wakageuka BOMBA LA NYOKO na WANAHARAMU!:-(


SAMAHANI ngojea nilainishe nyoko ya hoja hii!
Nacho jaribu kusema ni:

Muda fulani katika MAISHA,...
....Mtoto mzuri aliyezoea kusifiwa mzuri na watu....
...atakujashuhudia bado KUNA WATU mtu kibao tena ZA KUTOSHA wasiovutiwanaye ndipo atakapostukia JICHO kila mtu analo na hata kama unapenda nyonyo kama soksi iliyojaa maji kwa kuzipapasa , bado JICHO NI MWANAHARAMU!:-(

Na YUPO ambaye MUDA fulani katika MAISHA,...
...atastukia uzuri wake aliyekuwa anauona sana ni MAMA YAKE TU MZAZI na ajipendekezao kwao wanamuona ni mzuri kama harufu ya viatu VICHAFU vilivyoloa jana vya wenye fangasi watu....
... na awapaparikiao , KWA KUPAPARIKA hao watu BADO watadai kidude chake hakiwapandishi HAMU.

Ingawa pia YUPO atakayestukia katika muda fulani katika MAISHA,...
....alichotaniwa na kudhaniwa ni miguu kama za baiskeli SPOKU, matako mny'ong'onyeo au tu lile BICHWA kama tofali na watu....
.... ndio vilivyo kwenye CHATI sasa na kwenye fasheni kipindi hiki ,na sasa ni zamu yake kuchekewa kwa sana na linawavutia WALOKOLE mpaka WANAHARAMU.



Lakini KUMBUKA kuna MUDA katika MAISHA,....
...hata uwe MTOTO MZURI na ni kipenzi cha watu...
... utabaini KILA SIKU UNAZEEKA na MVUTO WA JANA si WA LEO kama UNATUMIA AKILI, na kama hutumii akili USISHANGAE ukijastuka wakati UREMBO WAKO UMESINYAA na WALIONOGEWA nawe JANA leo wamestukia yako IMESINYAA na hunogi tena kama JANA na KIPENGELE CHAKO kwao hakiwapandishi MDADI WA HAMU.


Na katika MUDA fulani katika MAISHA,...
...Mtoto mzuri kumbuka kubalansi ya Ubongo,KIMWILI na ROHO [AU kwa Kichina ya:''MIND,Body & Soul] wakati unahangaika na watu.....
....LA SIVYO usipoulisha UBONGO utaishi ukijisikia mjinga, usipolisha ya MWILI unaweza kufa kwa njaa uko uchi huku bado una nyege, na usiposhibisha YA ROHO, mapungufu yake yatasababisha UZIDI KUOGOPA kujisikia kufakufa na hapo ndipo WAJANJA hawakawii KUINGIZA GIA KUBWA katika kukutishia ya JEHANAMU.:-(

DUH nisikutishe !
Bado Mie MTAKATIFU Simon Kitururu na imani na uhusiano wa kati ya BINADAMU na WATU!



Swali:

  • Bado ya ukubwa hayajawahi kukusikilizisha KUFAKUFA?
  • Unakumbuka dakika hii unaendelea kuzeeka?

NALIKATIZIA WAZO hili NYOKO hapa!:-(!
KUMBUKA TU hili NI WAZO TU Mheshimiwa weye ULIYEWAHI KUWA Mtoto Mzuri huku MAPENGO!

Ngojea Lokua Kanza atulize mcheche kwa kitu-Salle


Au tu Cesaria Evora azidi kutuliza mchecheto kwa kitu-Sodade

Read more...

Nukuu za leo ni kutoka kwa Muammar al Gaddafi!

I cannot recognise either the Palestinian state or the Israeli state. The Palestinians are idiots and the Israelis are idiots.
Tafsiri kwa ung'eng'e mtaani: ''Waisrael na Wapalestina ni ndugu ukiingilia ya ndugu utachekesha!''



Libya has had to put up with too much from the Arabs for whom it has poured forth both blood and money.
Tafsiri mtaani:''Mie Muarabu lakini Waarabu kwa kuwa ni ndugu zangu bado kindugu wananizingua''



The times of Arab nationalism and unity are gone forever.

Tafsiri mtaani:'' Nanogewa na Umoja wa Afrika ulio kama gari Mkweche!''




There must be a world revolution which puts an end to all materialistic conditions hindering woman from performing her natural role in life and driving her to carry out man's duties in order to be equal in rights.
Tafsiri mtaani:'' Wanawake acheni kujaribu kukojoa mesimama kwa kuwa tu wanaume wanakojoa wamesimama HASA kama kitendo hakiendani na haja kubwa kwa kuwa staili ya kukojoa bado si kipimo cha usawa hasa kutokana na swala lenyewe liko kwenye KITENDO na sio staili ya KUTENDA.''

HABARI YENYEWE NDIO HIYO na MIE nimetafsiri tu alichosema Mheshimiwa Gaddafi kama mrindimo wake niusikiavyo mtaani!:-(

Aliyesema ni Muammar al Gaddafi na usinilaumu MIE babu wee!
[sentensi hii imeshikiwa kiuno na mwanadada]


Muammar al Gaddafi quotes nimezitoa kwenye Brainy quotes

Hebu basi tubadili hali ya hewa na kujiuliza kuhusu ukweli wa WIKIPEDIA tena...

Read more...

HISTORIA za mambo mengi zijulikanazo ni UONGO!:-(

>> Wednesday, September 02, 2009

[Tahadhari:Unaruhusiwa kunibishia!]


Kama wewe ni mchunguzaji wa tabia za watu utastukia karibu kila asimuliaye kitu,....
..... kuna uwezekano anaongezea CHUMVI STORI au anapunguza mpaka ujazo wa utamu wakitumbua . Kwa mfano stori yenyewe inaweza kuwa ilihitaji tu sentensi: ''KITUMBUA CHANGU UPANDE MMOJA kimeungua'' ,na anaweza akakusimuliwa MPAKA kuwa na mafuta yaliyotumika KUKIUNGUZIA kitumbua ni ya fisi. Na utakoma mwenyewe ukitaka akusimulie histori ya jinsi KITUMBUA kilivyogunduliwa kabla ya MAANDAZI!:-(

Na ukibadili mkao na kuwachunguza tena MTU KIBAO zikusimuliazo KITU,....
.... utazidi kugundua kuwa huwa mara KEDEKEDE wanakusimulia wapendavyo kuikumbuka stori na sio kama stori ILIVYOTOKEA kitu kisababishacho dunia kujaa HISTORIA MKWECHE!:-(


Haki ya njiwa tena!

Ukichunguza utastukia mpaka STORI ya KUMLA KUKU WA KIENYEJI hasa kama IMETOKEA asimuliaye ni MPENDA NYAMA YA BATA ,....
......STORI ambayo KIMILA inabidi IANZIE ...... alivyokimbizwa kuku VICHOCHORONI na hata alipokimbilia KIBANDANI ilivyobidi ndani ya kibanda ahangaike naye KABLA ya kumnyonyoa MANYOYA kuliko ruhusu JICHO lione vizuri UPAJA ULIVYO NONA kabla KIUMIO na kionjeo havija muhakikishia UPAJA ulivyo MTAMU,.....
.... kumbuka tu kama asimuliaye ni MPENDA NYAMA YA BATA , kama wewe NI MPENDA KUKU ,isikilize na fikiria mara mbili au zaidi kwa kuwa akusimuliaye stori hiyo kwa kuiita ya kuku anaweza akawa anakusimulia STORI YA KUMLA BATA ambaye kwake ni mtamu na ndio apendaye stori zake KUSIMULIA ingawa kwako huwa UNAANZA KUSIKIA KICHEFUCHEFU wala hata kabla hujaanza kufikiria maringo ya bata anavyotembea BILA VIATU na bila aibu anaenda msalani!:-([Samahani kwa kurefusha taralila:-(]


DUH!

Sipingi lakini umuhimu wa kujua HISTORIA ya vitu kwa kuwa inaweza kukurahisishia HATA kuelewa kwanini kwa WAHESHIMIWA WAKIAFRIKA au tu wadhaniwawo ni WAHESHIMIWA maeneo bado :

  • Wavaao BIKINI wasio na tako ni bomba na wavaa vibwaya pamoja na kuwa na bomba la tako la KISWAZI ni nishai!



  • Waafrika wakatao WEI kama lile la KAMBONA ni waheshimiwa na TUSIOCHANA Nywele na turasta TWETU ni nishai!

  • Keki na Mikate kwao bomba na Kula magimbi na viazi vitamu kwa chai NI nishai .

  • NA na nakadhalika kadhaa tatu na nusu unaweza ukajazia hapa...... na hapa......na...... ,au unaweza tu usijazie kitu kama unajisikia uvivu kidogo kama kawaida yako!:-(


KUMBUKA tu kuwa bado tunabishana kuhusu HATA histori ya MTU mpaka wajanja wanaweza kukulaani ukikana BINADAMU HAKUUMBWA na MUNGU hata kama WEWE huamini kuna MUNGU.

Na wengine wajanja watakusimulia historia ya mtu tokea alivyokuwa MJUSI mpaka alivyo geuka NYANI pale SERENGETI na kwa data ambazo sijazipata zote inasemekana MJUSI ALIPOFIKIA kuwa nyani hapo akagundua tendo la ndoa na kuzaliana mpaka akatoke MTU tena ni mitaa HIIHII ya Afrika Mashariki.

Tukiacha utani:

Na wasiwasi kama kweli MTU hakuumbwa na MUNGU kama HISTORIA fulani na tafiti za akina DARWIN zidaivyo na kutuhakikishia, basi Nyani wa kwanza kugeuka mtu kwa vyovyote VILE mchumba wake alikuwa bado ni NYANI.:-(

Swali:
  • Kama unaamini ya evolution basi si ni kweli yako Nyani aligeuka mtu?
  • Na kama unaamini uliumbwa na Mungu na wazazi wa kwanza wa binadamu ni Adam na Eva si maana yake unakubali lazima DADA alizaa na KAKA kipindi fulani wakati Nyumbani kwa Mzee Adam hakukua na jirani ?

  • Kwani usipojua historia ya JOGOO kuwa inaanzia kwa KUKU au YAI maana yake inachangia kukupunguzia utamu wa NYAMA YA KUKU/jogoo au inakukufanya uwe VEGETERIANI kisa hujui asili ya kifaranga?



Ni wazo tu PAPAA wa KUNESANESA na SISTA Mtanashati!
Labda kuna ukweli kwenye historia USINUNE BASI!:-(


Tupumzike Mtoto amwambie MAMA kitu katika-I don't like U Mommy


AU ngojea Artful DOdger ft Craig David warudie-Re Rewind


Au tu tubakie na Craig David katika kitu - Fill ME in

Read more...

YA WENGINE yakisaidia kukukumbusha YA KWAKO!

Unaweza ukampigia chabo CHEUPE DAWA,....
.... akafanya ujistukie kuwa weye ni CHEUSI DAWA kama mimi.



Na unaweza kuona tajiri,...
....ukakumbuka jinsi ulivyo masikini.

Unaweza pia kustukia WAKRISTO,...
....wakafanya ujifunze zaidi kuhusu UISLAMU.

Ila jihadhari tu kama kwako ukienda HAJA kunakukumbusha KULA,...
.... hasa kama CHAKULA na VIFYONZO/kilainisha kiu , NI vya kubahatisha au mipango na mikakati ya kuvipata leo tokea jana kulikuwa HAKUNA.


Nikiacha utani!:-(

Kama ukitumbulia macho wengine unajiona wewe,....
... au vyako hukusaidia kuwafikiria na kuwaongezea wengine, ...
....BASI kunauwezekano WEWE ni BOMBA la mtu na unastahili hata kwa mara nyingine kuchumbiwa au tu kupewa tendo walifuatilialo wachumba kama tu angalau ushasawazisha ya chumba !


NIMEACHA wazo na KUMBUKA HILI ni wazo tu KIBOSILE!






Swali:

  • AU?
  • Kwani ni lazima mpaka uwemtaani NA kwa bahati mbaya ufanikiwe kukipigia chabo KIFICHA NYETI/kitunza eneo cha mtu MWINGINE ndio ukumbuke kuwa wakati unavaa kabla ya MTOKO ulisahau kuvaa kificha nyeti!CHUPI?



Ngojea ukumbushwe MUHAMMAD ALI asili yake sio MBEYA au KILOSA bali eti ni Ireland



Samahani siku yangu iko fastafasta kidogo leo kama spidi na sauti ya Daddy Freddy katika-Haul &Pull



AU nafikiri ni kama Daddy Freddy katika-Bring the Girls

Read more...

Nukuu za leo NI kutoka kwa Idi Amini Dada!

>> Tuesday, September 01, 2009


“I am the hero of Africa.”
[Mi bomba la mtu Afrika]




“You cannot run faster than a bullet.”
[Kijeba ukitoka baruti huwezi shindana na mkuku wa risasi]

“If we knew the meaning to everything that is happening to us, then there would be no meaning.”

[Kama tungestukia maana za kila nanihii zitunanihizo , nanihii zingekuwa hazina maana]

“In any country there must be people who have to die. They are the sacrifices any nation has to make to achieve law and order.”
[Katika kila nchi lazima wawepo ambao itabidi waachie ngazi.Hao ndio kafara ya kusababisha nchi itulize mcheche]

“Sometimes people mistake the way I talk for what I am thinking.”
{Kuna wakati kuna mtu huchanganya jinsi navyolonga na kufikiri ndivyo navyo kuna kichwa]


Ni Idi Amin Dada quotes mie nimetafsiri tu kwa kiswahili fasaha cha mtaani kwetu.

Nukuu zote ni kutoka HAPA



Au ngojea tushangalie hii picha .....















AU tu twende Kenya Les Wanyika wakumbushie tena -DUNIA KIGEUGEU


Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP