Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Pamoja na yote BADO mdomo unauhusiano na TOBO!:-(

>> Thursday, March 12, 2009

Katika kurudia kuunganisha mahusiano ya vitu,....

labda......:-)...loves....:-(


...... sababu za kuweka MLENDA kwenye mdomo ni kulenga TUMBO na labda NIA ni kuufikisha tumboni , ingawa labda mdomo ni tobo la tumbo kama hujaziba TOBO.

Kinyeo pia ni USHAHIDI wakuwa TUMBO limetoboka, INGAWA unaweza kuendelea kubabaishwa na SIMULIZI za UTUMBO ukasahau uhusiano wa kinyeo na tumbo wakati tunazungumzia UMARIDADI wa KOO kabla ya TUMBO.

SIKUBISHII ukinibishia lakini!


Pamoja na yote,...
.....VITU karibu vyote vinauhusiano kama tu MIMI na WEWE ukiviangalia hata bila UMAKINI.

Swali:
  • Unakumbuka WEWE na MIMI tunahusiana?

Tatizo ni,...
.... katika vilivyotoboka, ni mpaka uwe na mtazamo au TABIA ya kuliangalia tobo na kuanza kufikiria uwezekano wa labda tobo LIMETOBOKA , iliKUGUNDUA labda si kweli kinyeo na mdomo vyote VIMETOBOKA katika huu uhusiano wa haya MAHUSIANO.:-(

Tatizo ni,...
....wakati unaulengesha mlenda kwenye TOBO la tumbo ,ni tatizo kama HUKUMBUKI kilengwacho na yote MARINGO na madahiro ya mlenda si tumbo bali AFYA YA MWILI.


NAACHA!
Kumbuka nawaza tu hapa na nakutakia kila la kheri chooni leo!

Siku Njema!


Swali:

  • Huwa unakumbuka kuangalia mahusiano ya UHUSIANO wa HIKI na KILE?
  • Unauhakika hujasoma ujinga PEKEE kama umefikia KUSOMA mpaka kwenye sentensi hii hasa kama HUWA huoni uhusiano wa ujinga na akili ?

Ngojea Manu Dibango abadilishe tena hali ya hewa katika-SOUL MAKOSSA

Au tu Manu Dibango alete za -Miss Cavasha

Read more...

Katika KUTETEA SURA nzuri isiyo na CHUNUSI isiyokumbukwa SURA!

Kumbuka....
...... hata kinyeo kina SURA wakati unafikiria SURA.

Na kwa kuangalia picha kubwa unaweza usiione SURA YA CHUNUSI kwenye SURA.

Lakini,...
.... SURA yenye chunusi .....

.....BADO ....
INAchunusi HATA kama AJALIYE MADOGO kwenye USO haoni ndita za chunusi kwenye SURA.

Unaweza kutetea uso kwa kusisitizia udhaifu wa kudumu kwa CHUNUSI kwenye SURA lakini!:-(

Kumbuka tu kutosahau kuwa,....
.... CHUNUSI nayo ina SURA.

Na,...
.. uso mzuri labda ulikuwa na CHUNUSI yenye SURA NZURI tu!:-(

Swali:
  • Ushawahi kujiuliza ugumu wa kutunza chunusi ibakie usoni?
----------___________________-----------------------------------

Nimeacha!
Kumbuka nawaza tu!


Ngojea Naughty by Nature watukumbushe- OPP

Au tu Fresh Jumbe aturudishe nyumbani katika -AMA ZAKE AMA ZANGU

Read more...

ANA macho, ngozi...na ulimi na KUKUPENDA kwa KUGUNA au MLIO!

Labda ni aibu KUKIRI,...
... udhaifu wa binadamu katika hisia mia ikiwa moja KASHIKILIA.


Labda ni aibu KUKIRI,...
.. kama mwenyemacho atumia dira ya mguno na kilio UKILIA.


Kwa maumivu au utamu katika KIKIRI,...
.....kakara maungo-tikisa na atahakiki ukiguna au KULIA.

Macho yanaona meno kama NGIRI,...
na ukikaa kimya hajui kapatia kama huguni au KULIA.


Ahitaji masikio kwa kuhakikisha yaonekanayo FIKIRI,...
... na wakati aonja kwa ngozi akiguna na KULIA.


Na mengi ya kuhudhunisha yapo FIKIRI,...
... na mengi wayaona ingawa wameacha kuguna na KULIA.


Labda bado watu wanahisia zote na watumia moja NAFIKIRI,...
....sababu za mengi ya kushoto bado yako kushoto na si KULIA.

Kama unagusa , kuonja,...na wasikia FIKIRI,...
.....wadhani si udhaifu ukitaka mpaka uone chozi ndio ujue mtu ANALIA?

-------------------------_________________________----------------------------


Nawaza tu USITISHIKE!
Swali:
  • Bado unafikiri unahitaji masikio uwenauhakika na unachoona kama macho yanaona?
  • Unafikiri unaona kwakua una macho na ulimi haukusaidii kuona kwa kuonja ukitaka kujua?


Naacha!
Namuachia Dr Alimantado katika -Best dressed chicken in town

Au tu Linton Kwesi Johnson azungumzie ya - Want Fi Goh Rave

Read more...

MBOLEA!

>> Wednesday, March 11, 2009

Labda ukiinusa inanuka,...
..... na ukiilamba ni SUMU.


Mimea huhitajika,....
....kwa mbolea kujisikia ina maana na si SUMU.


Akili zako hazina mpango kama mbolea zisipotumika,...
.... kama hazitumiki kumea hata kama mmea hauhitaji SUMU.


Na kama UBONGO usiotumika,...
....mbolea isiyotumika ni SUMU.


Mbolea!

.....labda UKIINUSA inanuka,....
.......................na ukiilamba ni SUMU.

Hata kama inatumika,....
.....ukiizidisha bado ni SUMU:-(

-----------------------------------------________________--------------

Nawaza tu usitishike!

Siku Njema!

Tutulie na kazi za mwanamuziki nipendaye kazi zake tokea enzi za Tony Toni Tone, Lucy Pearl na hata akiwa solo kwa jina Raphael Saadiq.
Hapa nimuache Raphael Saadiq,akiwa na Ali Shaheed Muhammad na Dawn Robinson.
katika...kibao....-without U

Au tu niiache kazi yake nyingine akiwa katika Lucy Pearl , kibao cha akinadada kusutana- Don't Mess With My Man

Read more...

LABDA kwa bahati nzuri WEWE ni MIMI!

Mimi sio wewe,...
... na yangu huyajui ingawa yangekupa KIWEWE.


Kuku sio Mwewe,...
.... na kicheche atakaye nundu anawezaishia kupata NGEWE.


Bado niko na wewe,...
.... ingawa hata kwa yangu tunafikiria ya WEWE.


Natulia kama wewe,...
...ingawa ninahasira na vurugu kama WEWE.


Nikichoka ninalala kama wewe,...
....ingawa ukilala ndotoni wasahau kuniona mimi ukijitazama WEWE.


Kumbuka pamoja na ujinga LABDA mimi ni wewe,...
...na yangu yaweza kuumiza yako WEWE.:-(


AU?
_______________________________-----------------_______________

Nawaza tu MKUU!
Ngojea Zhané waelezee matakwa katika - Hey Mr. D.J.


Au tu Manu DIBANGO azungumzie - Electric Africa

Read more...

HALELUYAH labda MWANAMPOTEVU hajapotea!

>> Tuesday, March 10, 2009

Swali:

  • Kama dunia yenyewe imepotea si labda mwanampotevu anapatia kwa UDHANIAYO ni kupotea?
  • Kama dunia inapatia unafikiri una ndoto za mbinguni za nini?

BAADAYE!
Swali:
  • AU?

Read more...

Kama UMESTUKIA unaweza na UNAJUA JINSI ya KUVUMILIA ukinyimwa na MALAYA!

>> Monday, March 09, 2009

WAKATI unaendelea KUVUMILIA wakati UMENYIMWA na MALAYA,....

.....bado....
AFRIKA inagawa kama malaya na kumnyima iliyomnyima liMTU kama ANYIMAVYO mtu MALAYA.


Labda,...
... AFRIKA ni BARA MALAYA ingawa kuna wanyimwao na MALAYA.


KATIKA.....
... KUVUMILIA ni bado unavumilia kwa kuwa ULITAKA na ukinyimwa ROHO INAUMA KWAKUWA ULITAKA ingawa uko katika uvumilivu na unafikiri imekuaje hunauhakika UTAPATA ya kawaida na unashangaa umenyimwa uliyofikiri ni YA UHAKIKA yake MALAYA.


Wakati UNAVUMILIA bado ni KWELI ulitaka kuifanya hata ambayo sio ya MALAYA ,na kunauwezekano unakumbuka au baada ya kunyimwa NDIO UMEKUMBUKA unaweza KUCHEUA mwenyewe na huhitaji MALAYA.

Swali:
  • Wakati unafikiria maendeleo umewahi kukumbuka kitu kiitwacho PUNYETO?

KAMA,...
.... unavumilia LABDA unafanya na uvumilivu WAKO NI DALILI za kubobea katika KUFANYA.

FANYA BASI!
Swali:
  • AU?
  • AU unanisubiri MIMI nifanye?

NA ni KWELI,...
.... mambo ya MALAYA MTAMU anajua aliyeonja na kula MALAYA.


NA,...
.... wengi waongeleao, KUPIGA KELELE au KUMZUNGUMZIA malaya,hawamjui MALAYA
Swali:
  • AU?
  • Kama AFRIKA ni demu mwenye chunusi unafikiri unge mtoa chunusi kwa kubinya chunusi au kwa kumsifia anachunusi ujualo halidumu kwenye uso mzuri?


NAACHA!


Ngojea nimuache rafiki yangu Papaa Kweba ofisini!Kweba eeh, unanitenga lakini!Tuko pamoja na salamu lukuki!
























Ngojea TONY HENRY alete tena muziki aina ya opera katika- NOW we are FREE.



Au ngojea TONY HENRY wa RNB alete za- Redemption Song


DUH!!
Basi tupate tu ZUKE kutoka kwa Jacob Devariux na wenzake...


Read more...

GHAFLA MTOTO kagundua kaota MAVUZI!

>> Sunday, March 08, 2009

GHAFLA mtoto ushahidi anao KAKUA,...
... na aweza kudhani ni wakati wakumbishia mvuvi UVUVI, kakua.



CHUCHU imenenepa KAKUA,...
... na aweza sahau walio na mvi chini ya kalikiti bado WANAMVI na walikua.


NI safari KUKUA,...
.... inataka muda kukua na ya miaka yataka miaka hata vile kama hutaki vile HIVI, utakua.

KUA mwanawane KUA,...
.... kama na una mavuzi usiwe na wasiwasi, SUBIRI yatapata MVI mavuzi ukikua hata bila MVI ukikua.

Ingawa mvi si kukua,...
....labda wahitaji ujue wapi pamenyolewa ingawa ni kipara UGUSACHO na unadhani hakina MVI hujakua.

--------------------------------------------------------------------

NAACHA!
Swali:
  • AU?
  • Unauhakika umekua?
  • Unauhakika unajua?
Twende tena SENEGAL kupata- bes bi sa bessa katika miondoko ya muziki aina ya Mbalakh




Au tu Gregory Isaacs katika - Rough Neck

Read more...

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP