Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

ANA macho, ngozi...na ulimi na KUKUPENDA kwa KUGUNA au MLIO!

>> Thursday, March 12, 2009

Labda ni aibu KUKIRI,...
... udhaifu wa binadamu katika hisia mia ikiwa moja KASHIKILIA.


Labda ni aibu KUKIRI,...
.. kama mwenyemacho atumia dira ya mguno na kilio UKILIA.


Kwa maumivu au utamu katika KIKIRI,...
.....kakara maungo-tikisa na atahakiki ukiguna au KULIA.

Macho yanaona meno kama NGIRI,...
na ukikaa kimya hajui kapatia kama huguni au KULIA.


Ahitaji masikio kwa kuhakikisha yaonekanayo FIKIRI,...
... na wakati aonja kwa ngozi akiguna na KULIA.


Na mengi ya kuhudhunisha yapo FIKIRI,...
... na mengi wayaona ingawa wameacha kuguna na KULIA.


Labda bado watu wanahisia zote na watumia moja NAFIKIRI,...
....sababu za mengi ya kushoto bado yako kushoto na si KULIA.

Kama unagusa , kuonja,...na wasikia FIKIRI,...
.....wadhani si udhaifu ukitaka mpaka uone chozi ndio ujue mtu ANALIA?

-------------------------_________________________----------------------------


Nawaza tu USITISHIKE!
Swali:
  • Bado unafikiri unahitaji masikio uwenauhakika na unachoona kama macho yanaona?
  • Unafikiri unaona kwakua una macho na ulimi haukusaidii kuona kwa kuonja ukitaka kujua?


Naacha!
Namuachia Dr Alimantado katika -Best dressed chicken in town

Au tu Linton Kwesi Johnson azungumzie ya - Want Fi Goh Rave

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 2:35 pm  

Simon,leo sisemi:-(

Simon Kitururu 7:46 am  

@Dada:Duh!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP