Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda tunapoteza UBORA wa SANAA ya KUSUTA na KUPIGA MKWALA!

>> Wednesday, March 18, 2009

Unaweza KUPANDISHIWA sketi wakati UNASUTWA kwa madoido wakati unashushiwa DALILI za tusi MURWAA na adaiye anakupa UKWELI !

Lakini,...
... ni MSAMIATI na mrindimo wa jinsi upewavyo MSUTO na MKWALA ndio hukamilisha FANI katika kuchojoa ugumu wako wa kuumizwa na MSUTO hata ndani ya MKWALA.

  • Sikubishii lakini kama unaridhika na MSUTO ukibaniwa pua wakati UNASUTWA au unapenda tu kukoromewa UKIPIGWA MKWALA katika kujali kwako USIKILIVU wa MKWALA kama MKWALA!

Chakusikitisha ni,....
.... sanaa ya jinsi ya KUSUTA au KUCHIMBA MKWALA inabidi ujifunze mwenyewe.

Na....
  • Hakuna TUISHENI ya kuchimba MKWALA!:-(
  • Hakuna twisheni ya KUSUTA!:-(
.....na darasani WALIMU hakuna!:-(


Uzuri wa KUSUTWA ni uwezo wake wa kukusaidia KUMFAHAMU zaidi AKUSUTAYE hasa kwa kuwa anakuambia mpaka asiyofikiri ANAKUAMBIA, na kukufaidisha kwa KUKUKUMBUSHA kitu kuhusu WEWE MWENYEWE katika DUNIA hii tuliyofikia KUTOJALIANA na kufikia kuendekeza VITA kutokana na kutojulia kumaliza ugomvi kwa MKWALA na KUSUTA wakati amani INABOA.:-(

Swali:
  • Hivi India na Pakistani si wamesaidiwa kwa KUPIGANA mkwala ndio maana bado vita haijaanza?
  • Unafikiri kwa mkwala unaUAhamu ya vita?
  • Unataka kusema hata kama si wewe uliyesutwa au kupigwa mkwala, hujawahi kustukia ULIBURUDIKA kushuhudia hizi SANAA?

Tatizo la....
.... kuchimba MKWALA, ukikosea MSAMIATI ,flooo na kushindwa KUMTISHA mtu, mnaweza ishia KUPIGANA VITA.:-(

Swali:
  • Hivi kusutana na mkwala sio TAYARI vita?


Naacha!
NAWAZA TU Mheshimiwa!
Hebu twende Tanzania CNN wajadili miundo mbinu...

Au tu Mwanadada wa Kichaga NAKAAYA alonge---

DUH tubadili hali ya hewa kwa kumuachia Mystikal awaamrishe watu fulanni...-Shake ya ASS[tahadhari lugha chafu kama wewe ni msikilizaji wa maneno kama yule]

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP