Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda UNAONJEKA!

>> Tuesday, March 03, 2009

Kuna watakaodai ukila si lazima uonje kama ladha hakuna, kama tu watakaodai shughuli ya leo muhimu ya viumbe ni kubugia ili kuishi hata kama kiumbe KINA kionjea ladha.

SIKUBISHII!!

NA,..
... wakati unajiandaa kujitetea kuwa huonjeki, WAULIZE minyoo na mafinyofinyo makaburini ni watu wangapi wameshawaONJA!:-(

Katika safari ya kumalizia safari ya umeumbwa kwa udongo na utarudi kwa udongoni , LABDA ni lazima uonjeke ili ugeuke udongo.:-(

Swali:

  • Hivi busara za majeneza ya chuma kama sio almasi kwenye kaburi la sementi si nikumuingilia Mungu na vipingamizi katika kuhakikisha alivyokuumba kwa udongo usirudi kuwa udongo?
  • Unakumbuka kama huna dhambi na ukafa bila kuwahi kufanya dhambi na kwenda mbinguni ,labda si utaanza kujiuliza utamu wa dhambi ulikuwa ni nini?

Wakati unadai huonjwi , usiende kwa daktari asije akahakikisha uogopacho kwa kusema kuna virusi na bakiteria vinavyokuonja sasa hivi hata kama hujisikii kuumwa leo kama jana!:-(

SAMAHANI KAMA ninakukwaza ingawa naamini kama unadini fulani kuna uwezekano ukatubu na kujisikia vizuri.
Swali:
AU?
Si dini ni za kuwasikilizisha watu VIBAYA au VIZURI kutokana na mahitaji ya mfuata dini?

SIku njeMA!


Namuachia Nusrat Fateh Ali Khan atupe muziki aina ya QAWWALI katika - Improvisation..

Au tu NIN na mshairi SAUL WILLIAMS wazungumzie- List of Demands

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:44 pm  

Simon kazi kweli kweli lakini tutafika tu bila shaka

Simon Kitururu 3:24 am  

@Dada Yasinta: Tutafika Tu!Kazi Kweli kweli!

Koero Mkundi 5:51 am  

Kaaaazi kweli kweli kaka Kitururu,

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 10:28 am  

wengi huonjwa kwa kudhani hawaonjwi. simoni wewe unaojaga / onjwaga je?

Simon Kitururu 1:15 pm  

@Koero: Siutani!:-(
@Kamala:Kwani wakati unaonja ni kweli unaonja au unafikiri unaonja?

Koero Mkundi 5:33 am  

Kuna chalii mmoja huku Arusha kamuanja House girl wa mjomba angu mpaka kaacha alama itakayofutika baada ya miezi tisa.
Yaani imekuwa soo.

Christian Bwaya 8:30 am  

Salaam mkubwa! Hatujawasiliana siku hizi mbili tatu.

Idumu JUMUWATA mkuu

Simon Kitururu 12:45 pm  

@Koero: DUH!
Bwaya:Salaam Salaam!Tuko Pamoja!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP