Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nyolinyoli! NAKUIBIA halafu SIFUNGWI!

>> Tuesday, March 17, 2009

LIONE VILE!
Linajua nilikuwa masikini!


LIONE VILE!

Linajua nina mshahara mdogo na halioni ajabu ghafla nina nyumba na magari ya kifahari yangu naniliyo mnunulia hawala yangu!


LIONE VILE!
Halafu litanipigia kura tena!:-(


LIONE vile hasa hili Litanzania!

Bingwa la kunyoshea vidole wengine wajinga na kwa amani likiendeleza ujinga!:-(

LIONE VILE ZURIIII, halafu NALIIBIA!


Wako ,
MWANASIASA -KIONGOZI.

P.S.
Naomba kura YAKO!


Swali:
  • Inawezekana sikuongelei wewe?
  • Ghafla kutajirika kihalali katika nchi tajiri kama Tanzania si inawezekana?


Ngojea BOB MARLEY azungumzie kitu katika -Running Away

7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 5:28 am  

Kitururu.

Haibiwi mtu hapa, siku hizi kila mtu ni mjanja......

Simon Kitururu 5:38 am  

@Koero: Sina uhakika haibiwi mtu wakati mchana mpaka umeme hatuna na kampuni ya Richmond ipo!


Wee hulali?Nakustukia kwenye net mida ya ajabu saa nyingine!Unatembelea kurasa za siri nini wakati watu wamelala?:-)

Yasinta Ngonyani 9:21 am  

Basi wakati umefika wa kuchagua viongozi wenye busara na wenye kuijali nchi yao sio kujijali wenyewe tu. Kazi kwelikweli:-(

Koero Mkundi 5:10 pm  

He! Kitururu, Unikome mtoto wa Kichaga,
Ni nani alikwambia natembelea kurasa za siri usiku wa manane?
Shika adabu yako!
Hivi wewe Ukojeeeee!!!!!!

Simon Kitururu 5:17 pm  

@Koero:DUH!

Nimekoma ingawa nilikuwa natania na sina uhakika kwanini haikueleweka ninatania. Nimekoma dume zima mheshimiwa dada!

Na sina uhakika nikoje:-(

Koero Mkundi 5:36 am  

Ahsante kwa kukoma, nami nilikuwa natania.

Unajua na mimi nilikuwa nakuchungulia na mara ghafla ukaja mzima mzima.
nyoli nyoli nimemchungulia kaka Kitururu usiku wa jana.......

LOL......

Simon Kitururu 12:42 pm  

@Koero: :-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP