Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HESHIMU MAFISADI kama ni UAFRIKA kuheshimu WAKUBWA!

>> Friday, March 06, 2009

Labda,...
.... WAAFRIKA TUNAHESHIMA mpaka TUKATAWALIWA.:-(


HESHIMA ni kitu cha bure na labda ndio maana inasemekana WAAFRIKA wanaheshima sana kutokana na ukweli kuwa heshima ni BEI CHEE , kama hukiri kuwa ni BURE, mpaka kwa heshima tunategemea vya BURE na kwa heshima ni MASIKINI kwenye UTAJIRI.



Na,...
.... ukisema WAFRIKA wanaheshima sana hasa KWA WENGINE kuliko WAJIHESHIMUVYO WAO, .....

.... naweza kushindwa KUKUBISHIA wakati NIMESHUHUDIA kuanzia WATU mpaka DINI ZA KIAFRIKA wasivyo na zisivyoheshimiwa na WAAFRIKA, na watafiti mpaka wa guenea worms wazinguao Waafrika wako au wanatoka UGHAIBUNI.

Labda ni kweli,...
....SIKU HIZI kuna wataalamu kutoka nje wa mambo ya AFRIKA wakati Waafrika tuko mstari wa mbele katika imani na tafiti za wengine kwa ajili ya WENGINE!:-(


Swali:
  • Hivi si HIP HOP ni bomba kuliko MDUMANGE, Mdundiko, CHAKACHA na TAARABU kwa pamoja?

  • Hivi unauhakika Taarabu na Mlimani park JAZZ BANDI ,ni miziki ya Kiafrika?

  • Hivi WAAFRIKA pamoja na kuuana unauhakika wana na wali-KUWA na HESHIMA?

Turudi katika hoja,.....

Wakati unataka KULETA ZA KULETA za kuwalaumu mafisadi wajanja MTOTO WEYE, kumbuka KIAFRIKA tokea enzi hizo TUNAHESHIMU WAKUBWA na tulitawaliwa salama SALIMINI kwa heshima.


HESHIMU wakubwa weye usije laanika bure wakati unajua kwa kuwa masikini ni rahisi zaidi kwenda mbinguni kuliko tajiri kupenya katika tundu la sindano, na ukikosa heshima UTALAANIKA.

Swali

  • AU?

  • Hivi unauhakika UKIHESHIMU utaheshimika hata na waheshimiwa wasiojua heshima ni nini?

  • Hivi unatofautisha kuogopwa na kuheshimiwa?


Nauhakika tu,...
... wakati WAAFRIKA kwa heshima TUNALALAMIKA, kwa kulala TUNATENDA na matunda yanaonekana katika mkao wa kuendelea kuujaza ulimwengu kwa KUJIFUNGUA akina totoz zenye majina kama MIKAELA na MIKA hata kwa Kihindu, Kiislamu na Kigagagigikoko .

MUNGU IBARIKI AFRIKA!

Au kama na nyie MIUNGU mpo na mna BARAKA kinamna , BARIKINI BASI AFRIKA na WAAFRIKA kama mbarikivyo wengine na acheni NOMA!

AAAGH!

NAACHA!
Kumbuka nawaza tu hapa MKUU na labda sitendi!:-(
wiKIENdi njEma!

Tulia na YERBA BUENA katika- Guajira

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP