Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

STIGMA na DOGMA!

>> Thursday, March 05, 2009

Unaweza kuogopa kuanguka hadharani kwa kuogopa STIGMA iambatanayo na KIFAFA ukianguka badala ya kuogopa MAUMIVU ya kuanguka , wakati kuanguka ni kawaida hasa kama umewahi kusimama au kutembea, ingawa kama WEWE ni mjanja , inawezekana ulishawahi kuanguka wakati umelala.

DOGMA zaweza kukusababishia usijiulize uwezekano wa uwepo wa MUNGU WENGI au SHETANI WENGI kutokana na kuaminishwa kuwa kuna ukweli mmoja na ukweli wenyewe ni kwamba kuna MUNGU MMOJA mzuri na SHETANI MMOJA mwenye sura mbaya.



Labda,...

  • kuna ambaye hafanyi kitu ingawa kinafanyika kwa kuogopa STIGMA.

  • HAKIPINGIKI kitu ingawa kinapingika kwa sababu ya DOGMA.


Labda,...
  • DOGMA ni kukana MACHALE yako!
  • STIGMA ni kuogopa yako TAFSIRI ya machale yako , kwa sababu jamii inatafsiri na kuoanisha tafsiri na kitu .Kitu uofiacho kinakuathiri!


Dosari za stigma ni pale wewe mwenyewe utakapofikia kuamini waaminiyo kuwa ni dosari hata visivyo na dosari kwa sababu kuna stigma iliyojengeka katika jamii hata kama ni ya kuoanisha kula sana na ulafi hata kama kazi yako ni mgonga kokoto na umbo lako ni kubwa kuliko, na sahani kubwa inakuja na hali halisi na si kwa ulafi kwako .

Dosari za DOGMA ni ukweli kuwa ni mtu mwingine yalimshinda kuelewa na kuelezea KWA NINI, na kaamua kuwa HIYO iwe ndio kweli tupu kwa wengine wote na USIBISHE.

Labda,...
.... katika kulainisha mambo ya STIGMA unaweza kuunganisha na ya jamii ya KiTZ ya kama labda :

  • Ukibana matumizi na kama wewe ni MPARE kama mimi, watu wataendelea kufikiri wewe ni BAHIRI kwa sababu Wapare wana STIGMA ya ubahiri.

  • Hata kama wewe tajiri , ukiomba halafu ikajulikana wewe ni MGOGO, watu wataamini kuomba kwako kuko kwenye damu kwa sababu kuna waaminio ombaomba ni Wagogo.

  • Ukiiba kama wewe MCHAGA kama watani zangu, kuna watakaodhani unatunza na kudumisha MILA na DESTURI kutokana na STIGMA iwalengeshayo Wachaga na wizi.

  • Tukipenda ngono kama WEWE halafu ikawa sisi ni Wahaya , LABDA kuna....
  • Nakadhalika tatu katika stigma na....


Na maswala ya DOGMA yanaweza yakakuchanganya hasa katika mambo ya dini ambapo usipoangalia utashindwa kuelewa akusimuliaye kuna MUNGU MMOJA lakini hapo hapo kuna Mungu Baba, Mungu Mwana na Mungu roho Mtakatifu , wakati unamsikiliza adaiye yeye kapatia kwa kuamini kuna MUNGU MMOJA na SHETANI MMOJA katika ya Mungu mengi na ya Shetani lukuki.

Swali:

  • AU?
  • Kwani STIGMA ni mpaka iwe ya UKIMWI au UKOMA mtaani na DOGMA aamue PAPA wa Kiroma VATICAN?

Katika STIGMA labda kunamchango wako kama unasaidia kuamini kuwa kuna dosari ambazo zinamng'ang'ania mtu daima na kwa mahesabu yaleyale uliosimuliwa ni MAHESABU ambayo ukitekenya lazima yazae DOSARI.

Katika DOGMA , sema unataka tu kurahisisha ili kujisaidia usijishughulishe kuelewa tofauti.

Swali:
  • AU?


STIGMA na DOGMA
DOGMA na STIGMA
......na labda vyote ni UJINGA.:-(

NAACHA!
KUMBUKA NINAWAZA tu hapa!
Nakutakia mafanikio MEMA NA MAKUBWA chooni leo!


Tutulie na Dave Chappelle alete busara za kukojoa katika- Piss On You


Au DAVE Chapelle aendelee katika- NIGGAR FAMILLY


AU tu Burning Spear a kumbuke katika -Days of Slavery

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP