Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Wakati KUNA vitu JAMII INAENDELEA kuamua ni MWIKO KUVIONGELEA kama tu KUCHEZEA mavi!

>> Sunday, March 01, 2009

Ni kweli,...
.....CHA AJABU ni kwamba jamiii imeamua kukataa mambo fulani yasiongelewe.

Lakini,.....
......MAMBO yanaendelea KUFANYIKA katika jamii ingawa hatutakiwi KUYAONGELEA.

Tatizo ni,....
.... jamii na JAMII hutofautiana na MIIKO ya jamii moja ni ruksa katika jamii nyingine.

Wakati jamii moja ni mwiko adhabu ya KIFO, nyingine kifo ni jambo la kawaida na KAMA WEWE MWANAFUNZI ukiandamana, hukawii kupigwa virungu na ukifa poa tu.

Na,...
....kuna JAMII ziaminizo ni mwiko kula kwa mkono kama tu waaminio kula kunahitaji KIJIKO, UMMA na KISU.

Swali:

  • Hivi JAMII ndio akina nani kama wewe hauhusiki?
  • Si labda KUTAWAZA msalani ni kuchezea mavi ingawa ni mwiko kuwa na huo MTAZAMO katika JAMII?

Miiko NI KIBOKO na inaweza kumfanya MUISLAMU ajifanye MLOKOLE kama jamii ni ya KILOKOLE.

Na,....
..... MWANAKIJIJI anaweza kufikiri ni lazima ajifanye ni MTOTO wa MJINI kama anahisi kuna MIIKO inayomkumbusha kuwa hayuko KIJIJINI kama tu Msenge ajaribuvyo kujifanya basha maeneo mengine.

WAKATI katika jamii MIIKO inaweza kumfanya MKATOLIKI ASIKIRI kaokoka, MLOKOLE anaweza akamkana YESU katika kusawazisha ya KIDUNIA kama ya KUOPOA NGOMA.

Labda,...
.... sababu za MENGI kutoongelewa ni fikra kuwa:
  • SI heshima KUNONG'ONEZA
  • SI busara KUONGELEA
  • NI aibu KUSEMA
  • NI matusi KUSIKIKA

AU
....LABDA hatuna uhakika na MAANA ya UYASEMAYO nayanachangiaje katika MUONEKANO WAO katika JAMII hata zaidi ya MUONEKANO WAKO.


Tatizo ni,....
...... ukichukua muda kufikiria ni kwa nini jamii INAMTISHA mwanaJAMII , unaweza kugundua ni kwa sababu MWANAJAMII HUTISHIKA.

Swali:
  • Unakumbuka lakini kuwa hata ukianguka sokoni kwenye UMATI wa watu , ni asilimia ndogo sana tu ya watu inayoweza kushuhudia UMEANGUKA au hata kukumbuka ULIPIGA chini?

  • Ushawahi kusikia AIBU kwa afanyayo MTU mwingine wakati hakuhusu na afanyayo HAYAKUHUSU?
  • Kwanini?

  • Ushawahi KUJIPENDEKEZA kwenye sifa za MWINGINE hata kwa kudai unauhusiano naye au mnatoka kijiji kimoja wakati HAKUHUSU na yake HAYAKUHUSU?

NAJUA baadhi ya niandikayo hapa kijiweni KUNA waaminiyo hayafai kwa kubwa zima KUONGELEA.

Lakini narudia,....
.... JAMII zina TOFAUTIANA kutokana na wanajamii KUTOFAUTIANA.
......JAMIII zinaendelea KUTOFAUTIANA kutokana na WANAJAMII kuendelea kutofautiana.


Na,....
......JAMII zilizotofauti ZINAENDELEA kuungana hasa kwa jinsi DUNIA inavyozidi kugeuka KIJIJI.

Usishangae kupigwa BUTWAA kila kukicha kwa kushuhudia MIIKO ikivunjwa kuanzia kwenye TV yako sebuleni mpaka kwenye uchochoro wa pembeni ya KANISA lako , MSIKITI wako , SINAGOGI lako au PALE uchochoroni, pale kati ya BAFU na CHOO chako.

Lakini,...
.... MIIKO ni gundi ya jamii na kama unavunja MIIKO kaa katika mkao wakujua kuwa BINADAMU ni king'ang'anizi wa MIIKO aliyoizoea imfanyayo aamini ANAELEWA na KUJIELEWA.

UKIVUNJA miiko unaweza ukawa ni tishio katika JAMII na BINADAMU kama MBWA KOKO , si kila mara ukimtisha anakimbia.

Mara nyingine BINADAMU kama MBWAKOKO ukimtisha akajisikia unamuweka kwenye KONA , anaweza kukung'ata MAENEO kama MJUSI tu.

Swali:

  • LEO umekwepa KUONGELEA mangapi kwa kuhofia JAMII itakuelewaje?
  • SI unakumbuka JAMII inaweza kuwa MAMA, Baba, DADA, Kaka, Mchumba, Kimada, Rafiki wa Mpenzi wako utamaniye KUMKONYEZA,.....na WEWE?


Tukumbuke tu LABDA,...
.....katika JAMII kuna wakwepao NYAMA YA NGURUWE na kula YA MBWA, kama tu ambavyo wapo wakwepao NYAMA YA MBWA na kula YA POPO . Na hata kama mambo yote ni MCHICHA , mwiko wako wa kula PEREGE labda haumuhusu mwenye mwiko wa kula SATO kwa CHUNGA.

SHIKILIA yako yenye MAANA kwako, YA wengine kama hayakuathiri wewe WAACHIE wenyewe WAHUSIKA hata kama yaletayo maana kwa WAHUSIKA ni KUCHEZEA mikojo.

Swali:
  • Miiko ya Mkatoliki Itali unafikiri inafanana na MIIKO ya Mkatoliki TANGA?
  • Miiko ya MUISLAMU Yemeni unafikiri inafanana na MIIKO ya Muislamu KAGERA?
  • HIVI miiko yako SEBULENI inafanana na ya CHUMBANI?
  • Hivi DINI yako sio KIONGEZO cha mkusanyiko wa MIIKO yako na labda SI lazima wengine IWAHUSU?


NAACHA MAHUBIRI!
Topiki imenishinda!:-(

Twende South Africa kuangalia somo katika -Music and apartheid in South Africa


Au tu huko huko South Afrika , Black Mambazo & PJ Powers wazungumzie -Knocking on Heaven's Door

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP