Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Pamoja na yote BADO mdomo unauhusiano na TOBO!:-(

>> Thursday, March 12, 2009

Katika kurudia kuunganisha mahusiano ya vitu,....

labda......:-)...loves....:-(


...... sababu za kuweka MLENDA kwenye mdomo ni kulenga TUMBO na labda NIA ni kuufikisha tumboni , ingawa labda mdomo ni tobo la tumbo kama hujaziba TOBO.

Kinyeo pia ni USHAHIDI wakuwa TUMBO limetoboka, INGAWA unaweza kuendelea kubabaishwa na SIMULIZI za UTUMBO ukasahau uhusiano wa kinyeo na tumbo wakati tunazungumzia UMARIDADI wa KOO kabla ya TUMBO.

SIKUBISHII ukinibishia lakini!


Pamoja na yote,...
.....VITU karibu vyote vinauhusiano kama tu MIMI na WEWE ukiviangalia hata bila UMAKINI.

Swali:
  • Unakumbuka WEWE na MIMI tunahusiana?

Tatizo ni,...
.... katika vilivyotoboka, ni mpaka uwe na mtazamo au TABIA ya kuliangalia tobo na kuanza kufikiria uwezekano wa labda tobo LIMETOBOKA , iliKUGUNDUA labda si kweli kinyeo na mdomo vyote VIMETOBOKA katika huu uhusiano wa haya MAHUSIANO.:-(

Tatizo ni,...
....wakati unaulengesha mlenda kwenye TOBO la tumbo ,ni tatizo kama HUKUMBUKI kilengwacho na yote MARINGO na madahiro ya mlenda si tumbo bali AFYA YA MWILI.


NAACHA!
Kumbuka nawaza tu hapa na nakutakia kila la kheri chooni leo!

Siku Njema!


Swali:

  • Huwa unakumbuka kuangalia mahusiano ya UHUSIANO wa HIKI na KILE?
  • Unauhakika hujasoma ujinga PEKEE kama umefikia KUSOMA mpaka kwenye sentensi hii hasa kama HUWA huoni uhusiano wa ujinga na akili ?

Ngojea Manu Dibango abadilishe tena hali ya hewa katika-SOUL MAKOSSA

Au tu Manu Dibango alete za -Miss Cavasha

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 3:10 pm  

Vituko, vituko, vituko haviishi Simon. Haya, ndiyo nakumbuka wewe nami tuna uhusiano we kaka na mimi dada:-)

Jingine chooni kazi kwelikweli:-(

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) 7:53 pm  

Ati - matobo yote aliyonayo binadamu yangezibwa, ingekuwaje? Mimi nadhani binadamu angeweza kuishi milele...

Simon Kitururu 7:43 am  

@Dada Yasinta: Asante kwa kutonitenga. Samahani kwa maswala ya kufanikisha CHOO kama yanatia HUZUNI!:-(

@Profesa:Nahisi inaweza kuwa kweli usemacho!:-(

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP