Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Nimewahi KUONA mtu MWEUSI , na LABDA SIJAWAHI kumuona mtu MWEUPE!

>> Saturday, March 07, 2009

Labda,...
....unapenda rangi ya JIPU LIKIIVA au tu rangi ya NUNDU kesho yake baada ya kupewa NUNDU.

Na,...
.... inawezekana WEWE ni MBAGUZI kama unauhakika wa MAANA YA UBAGUZI ni nini.:-(

Swali:

  • Kama unajua RANGI , kwa kawaida unazungumzia RANGI GANI nyeupe ya MTU kama katika SIMULIZI zako za karatasi JEUPE unazungumzia NYEUPE?
  • Ushawahi kuona mtu BILA rangi wakati unaangalia mavuzi au masharubu CHOMACHOMA ya MTU?[Samahani kama jina la nywelenywele nyingine inawezekana ni matusi.:-(]
Lakini,..
.....katika kuona KIBOGOYO unaweza kukumbuka MENO na ukajifanya ni kawaida yako kupiga MSWAKI wakati meno yako yameoza na yana rangi ya DHAHABU -MAVI.

Swali:
  • AU?

Na,..
... wakati unaona RANGI YA BLUU BAHARINI,ni KWELI inawezekana ukasahau BAHARI HAINA RANGI BLUU na uonacho BAHARINI ni rangi ya anga la BLUU.:-(

Swali:
  • Kama wewe ni MTANZANIA unauhakika MZUNGU na ALBINO wanatofauti YA uweupe wa rangi wakati kwako MAALBINO ndio DILI?
  • Unauhakika unajua JINA la rangi yako?

NAACHA!

Ngojea tutulie kwa kwenda CHINA kushuhudia mwanamama AKILIA kwa kuchelewa ndege......


Au TYRA Banks anisaidie kwa kujishebedua katika-Shake YA body

Au tu Whitney Huston arudishe UMAHIRI ingawa ni UONGO katika - I will always LOVE U

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 11:29 am  

Ndiyo kaka Simon kuhusu rangi;- rangi ni rangi kwani mweusi au mweupe ni rangi tu kwa sababu ukichukua kisu na kukata kitakachotoka ni damu nyekundu kwa wote yaani aliye mweupe na aliye mweusi. Hivi ni mtazamo wangu mimi mweusi

Anonymous 2:03 pm  

mKuu
amani kaka.

Mzee wa Changamoto 3:05 pm  

Si huwa wanasema kuwa kuna matatizo ya kuona rangi? Lakini weusi na weupe watokana na nini? Wanasema weupe ni kupungua ama kukosa pigment fulani hivi. Yaani upungufu wa wenzetu, sisi kwetu ni heshima. Mmhhhhhhhh
Tofauti ya Albino na Mzungu? Ni ujinga wa kichwani kuwa kuna tofauti hata ya mweusi na mweupe. Kama da Yasinta alivyosema na kama alivyoimba Da Khdja Nan kuwa kama unataka kubagua, basi m'bague binadamu kwa rangi ya damu.
See you next ijayo

Christian Bwaya 3:49 pm  

Ukichunguza sana utagundua kuwa kila mtu ni mbaguzi.

Tatizo la wale wa Afrika ya kusini walikuwa wawazi zaidi.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP