MKE mmoja, MME mmoja NA matamanio MAWILI na nusu!
>> Tuesday, March 03, 2009
Mke mmoja, Mume mmoja MTAMU!
.....Wakati ananoga,....
kikunogeacho hakiongezeki utamu UKINOGEWA.
Mume mmoja, Mke mmoja MTAMU!
.... Akiacha kunoga,....
kikunogeacho bado kitamu ingawa MWANABIBI kaacha kuonja na chakulambia,
......kama alivyokuwa akionja wakati tamu AKINOGEWA.Mke mmoja, Mume mmoja hakuna UTAMU!
---Hakikuwepo kinachonoga...
hakikuwepo katika mhusika tokea mwanzo, ingawa MABURUKI adai
......kilikuwepo na utamu ALINOGEWA.Mume mmoja, Mke mmoja vuguvugu UTAMU!
.....Mapungufu ya kunoga ....
ingawa Mme yupo na Mke yupo na bado mawazoni ni KITU- FANTASI ya mhusika wa tatu,
....kitu kikusogezeacho utamu UKINOGEWA.Mke mmoja , Mme mmoja.
Mme mmoja , Mke mmoja.
Mme mmoja , Mke mmoja.
.... Mawazoni una watu wangapi?
Mtu mmoja na Limchumba moja ndani ya UTAMU!
... Utamu wa wawili ukinoga,....
jumla ya utamu bado ni elfu tano,
jumla ya utamu bado ni elfu tano,
... na LABDA ndoa bado zipo hata mmoja USIPONOGEWA.
-------------------------------------------------------------------------------------
NAACHA!
Kumbuka nawaza tu na usitishike usiponielewa ingawa labda kuna watakao nielewa naongea nini kinamna!:-(
Swali
- Hivi mpenzi wako UBWABWA ni mzuri na anakaribia kufanana na yule umpendaye AKILINI-MUKICHWA au katika fantasi za WALI?
- Hivi unauhakika ndoa ni zaidi ya neno ndoa wakati bado MWILI WAKO uko kwenye ndoa na MAWAZO YAKO yameacha MWILI na YANAJARIBU ndoa IENDELEE kufanana na uaminicho ni ndoa?
- Mke mmoja Wanaume sita si ni NDOA kama ilivyo kwa Mume mmoja Wanawake ishirini na nusu?
- Hivi mchumba ni mtu?
Samahani naenda kukojoa!:-(
Baadaye!
Ngojea Teddy Pendergrass azungumzie - My Greatest Inspiration
Au turudi tu tena Ethiopia kukutana na TEDDY AFRO atulize mshawasha akisema- JAH
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment