Watu WEUSI wadhaniapo MWENYE ROHO MBAYA ana ROHO NYEUSI!
>> Monday, March 02, 2009
Kuna WATU WEUSI wafikiriao na KUAMINI rangi nyeusi ni ishara ya kitu kibaya kama tu wabaguzi wa watu weusi wajaribuvyo kuwaaminisha watu kuwa MTU MWEUSI ana kasoro na ni MTU MBAYA.
Swali:
- Si umecheki walivyofanikiwa eeh?
Unaweza mpaka kuwasikitikia WATU WEUSI ambao wanadiriki mpaka kutamka kuwa RANGI NYEUSI nishai na ni rangi ya mavi kwa mapungufu yao ya kugundua kuwa mavi yana utajiri wa rangi nyingi.
RANGI na MAANA ZAKE hutofautiana karibu kila mahali.Kuna nchi rangi nyekundu ni mbaya na inaashiria maovu wakati katika jamii nyingine rangi hiyohiyo ina ashiria MAFANIKIO.
Swali :
- Samahani kwakukuuliza; lakini hivi unafikiri tokea uzaliwe mpaka leo umefanikisha vinyesi vya rangi aina ngapi?
Tukirudi kwenye hoja........,
Kuna watakao sifia suti NYEUSI kama tu Benzi JEUSI kuwa zina rangi ya heshima na mafanikio, wakati wakikataa kuitwa WEUSI kwa sababu za;
- Weusi
- Giza, Usiku, -Maana yake huoni vizuri.
- Mtu mweusi ,-maana yake si mweupe.
- Nguvu za giza, nyeusi ,- maana yake ni za shetani.
na..
...nakadhalika tatu na nusu, ya kitu kilichowatoa kujiamini kwa kuwa WEUSI .
Swali:
- Umeshastukia KIDUME mpenda ngono hupenda kuiingiza kitu sehemu za giza asizoziona vizuri kwa furaha na hahitaji tochi?
- Hujawahi kugundua nguvu waziitazo za GIZA hufanyika zaidi MCHANA kwenye mwanga?
- Bado unaamini shetani ni mweusi na JINI ni mweupe?
Kumbuka SIRI ya DUA la KUKU kutompata MWEWE ni ukweli Mwewe hana imani na hajui kalaaniwa na KUKU.
WAKATI Mtu MWEUSI.....
.... anaamini UWEUSI ni LAANA , labda kwa AAMINIYE inakuwa kweli LAANA.
Cha kufurahisha,...
.... tupo ambao tunajua kuwa kuna ulaini pia uletwao na kuwa MWEUSI.
Cha kusikitisha ni,...
.... WAPO waaminio kuwa kwa kuwa WEUSI wamelaaniwa na watakao tumia mpaka vitabu kama BIBLIA kuhalalisha.:-(
Swali:
- Kama hakuna aliyewahi kuona ROHO, WEWE kakuambia nani kuna WENYE roho NYEUPE au ya RANGI ya MAVI?
NAACHA!
Siku Njema!
Tubakie Mozambique kwa André Cabaço ...
Au twende tena Cape Verde tukapate- Music Mix...
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Hivi tunajuaje kuwa nyeusi ni nyeusi kama tunavyodhani na wala sio nyeupe? Tunajuaje kuwa nyekundu ndio nyekundu? Kwa nini njano isiwe kijani?
Haya maamuzi ya rangi yanatokana na macho yetu ama 'kilichokichwani'?
Kwa sababu inawezekana rangi isiwe kile kinachoonwa na macho bali kile kinachojengwa na mawazo?
Cheusi au cheupe vyote ni sawa. Ila ukishaamua kuwa kuna tofauti basi iwe hivyo:)
@Bwaya: DUH! Hivi tunajuaje MTU ni mtu na ajulikanaye kama MTU sio NYANI?Kazi kwelikweli!
@Yasinta: Kazi kwelikweli!
Post a Comment