Wivu SINA , lakini sijui NAFIKIRI au NAHISI !
>> Friday, March 20, 2009
Kama unaamini huna WIVU,...
..... labda USIOMBEE kugundua GHAFLA una wivu USIJE ua MTU na BATA WAKE ghafla!
Na,..
...kila siku TUNAFIKIRI na KUHISI.....
Swali:
- Unakumbuka kufikiria UNACHOFIKIRIA na kukumbuka ULICHOFIKIRIA jana na KUKIFIKIRIA tena leo?
- Unakumbuka huwa HUKUMBUSHWI kuhisi?
Ukifikiria sana, LABDA unavyofikiri unavifikiria bado UNAVIHISI.
Na,...
....labda kama unafikiria HUNA wivu, basi wivu wako LABDA umelala na sina uhakika kama ni afya uuamshe udinde au tulia katika mkao huohuo wa sina WIVU ubakie umelala kwa utulivu!
Swali:
- Au unahisije wewe baada ya kufikiria hili?
Labda kuna UKWELI kuwa ,....
...kila mtu anastaili na mkao wake wakusikilizia WIVU.
Labda kuna UKWELI kuwa,...
...kuna mwenye wivu na MKE WAKE na mwenye wivu na SEHEMU ZA SIRI za mke wake.
Na labda,...
..... wakati SHOGA anakuonea wivu , HATAKI KULA vyako, bali anataka usiwenavyo ULAVYO ili apate nafasi ya KUKUTETA kwa kisauti kisikikacho kikisema; ''Sasa tulione litaringia nini sasa hivi wakati HALINA NANIHII, lione vile mwanya kama PENGO!'', halafu wala ASIMENDEE ulichokuwa una KULA kwa rahaaaa!:-(
Swali:
- Si unakumbuka roho ya kwanini?
SINAUSHAHIDI!
Lakini,...
... naamini unaweza UKAHISI halafu UKAFIKIRI bado unafikiri wakati UNAHISI tu utakiwacho SASA HIVI KUJUA baada ya KUFIKIRI na KUHISI.:-(
Swali:
- AU?
wiKIENdi njEMa!
Pumzika na Francky Vincent akizungumzia- Fruit de la passion
Au tu na Zouk Machine katika - maldon
7 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
DUH! KAKA KITURURU,
SIKUJUA KAMA UNA WIVU!
wivu wivu, maweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
sijui kama mimi ninao japo kunawenyenao kwangu
Bila wivu hakuna maendeleo:-(
@Koero:Nina wivu tatizo wivu wangu unaweza usistukiwe kwa kuwa kwa watamanio maandazi au keki kwa chai wakati huo mie natamani ukoko wa bamia kwa uji.
@Kamala : Endelea kuchunguza usije kugundua ghafla wakati unakojoa halafu ukamkojolea mtu bure!
AU?
@Dada Yasinta:Kuna ukweli! Halafu shauri yako kwa kuongea ukweliukweli kila wakati!
AU?:-(
mkuu soma hapa kaka
uchambuzi.blogspot.com
duh.
rasta hapa
Habari za hapa.
Nimepita hapa kibarazani kwako kujitambulisha kuwa nimefungua kijibaraza changu kitakachokuwa kikijihusisha zaidi na masuala ya vijana.
Nimekuwa ni msomaji wa blog yako kwa muda mrefu, na sasa nimeamua na mimi nijitose uwanjani ili kuongeza mchango katika kuielimisha jamii.
Niko tayari kuelimishwa na kukosolewa pale nitakapoonekana natoka nje ya mstari.
Natarajia ushirikiano wako.
Digna
@Rasta: Nimesoma!
@Digna:Karibu Digna! Tuko Pamoja!
Post a Comment