Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika SAYANSI ya KUKUBALIWA!

>> Tuesday, March 17, 2009

Si lazima uombe,....
.... lakini wahitaji KUHITAJI ili uvumiliwe na UKUBALIWE.

Unaweza kujichukulia kwa nguvu lakini,...
..... na watu wakaelewa baadaye kwanini ulijichukulia na UKAKUBALIWA.

Daima,...
....KUKUBALIWA kwako kunauhusiano na mahusiano yako ya MATAKWA yako na watu wengine.

La sivyo huhitaji KUKUBALIWA!

Na hata,...
.... katika taaluma ya kutongoza UNAHITAJi mtongozwa ili UKUBALIWE YAKO katika mtongozo.
Ila katika ,....
.. taaluma ya MAHUBIRI, ili YAKUBALIWE unahitaji kubobea kwa YASIYO YAKO UHUBIRIYO utakayo KUKUBALIWA.


Kumbuka,....

  • NI YAKO ya kutongozea UKUBALIWE!
  • NI YA WENGINE utumiayo KUHUBIRIA ukubaliwe!


Swali:
  • Katika KUKUBALIWA unafikiri wewe ni MTONGOZAJI au MHUBIRI?
Cha muhimu ni,...
.....kumbuka kukubali KUJIKUBALIA.

Wengi hata bila sababu za msingi hawata KUKUBALIA na kumbuka sababu yake kubwa ni kwamba HAWA JAMAA ni WATU bin BINADAMU.

Wasikilize lakini WAKIKUTONGOZA au KUKUHUBIRIA halafu kama unaroho nzuri WAKATALIE.

Swali:
  • AU?
  • AU unafikiri hujakubaliwa hata na MUNGU wa upendo?
NAACHA!
Tulia na Percy Sledge azungumzie jinsi mwanamme akipenda katika - When a man loves a Woman.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP