Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Labda UKITEKENYEKA ulikuwa tayari KUTEKENYWA!

>> Wednesday, March 18, 2009

Hutekenyeki NG'O kama hujakaa mkao wa kusikilizia MTEKENYO!
Swali:

  • AU?
Na akupendaye...
...... ukimstukia anafurahia ukicheka AKIKUTEKENYA, unaweza kujifanya UNATEKENYEKA mpaka UKAJISTUKIA mwenyewe jinsi ulivyobarikiwa UIGIZAJI MZURI kwa kuangua kicheko mpaka UKABANJA KIDOOOGO , wakati umeguswa GOTI wakati UKWELI ni kwenye KIKWAPA , chini kidogo ya KITOVU na kwenye wigo wa KIUNO , karibu na mipaka ya shanga TU ndiko UNAKOTEKENYEKA mwanawani weye na GOTI lako linauma.


Na,...
...HAICHEKESHI kama hakuna KITU KINGINE ukijuacho kisababishacho HIKI kikuchekeshacho udhani KINACHEKESHA.


Na,...
......AKUTEKENYAYE ukacheka, kunauwezekano umemruhusu AKUGUSE MWILI na KITEKENYEO ndio maana KAKUTEKENYA ukacheka badala ya KUMPIGA NGUMI pana, KONZI la nguvu, au tu KUMPIGA NGWALA baada ya KURUKA KICHWA , na wakati UMEMPIGA ROBA ukawa unaachia MSONYO MREFU na TUSI LENYE UJAZO ambalo kama sio la nguoni lihusianalo na mama yake, basi ni lile lifananalo na ;'' Mende wee nenda katekenye kuku wenu hukohuko! Nyooo !Lione vile!''


Na,..
...AKUCHEKESHAYE bila kukugusa , kuna uwezekano UNAMSIKILIZA au KUMUANGALIA kitu ambacho siku hizi kinasahaulika duniani, mpaka imefikia siku hizi BIN-ADAMU WENGI kufikia kupeana MPAKA mimba BILA KUANGALIANA na kabla ndoa haijafa, HAWASIKILIZANI.:-(


Swali:
  • Unakumbuka ulimi pia ni kitekenyeo?

Kumbuka tu kuwa,...
...UKIJIWEKA TAYARI , kumbukumbu hata za ulivyowahi KUTEKENYWA zinaweza KUKUCHEKESHA au KUKULIZA!:-(

Na kumbuka,...
... UKITEKENYWA sana UTALIA:-(


NIMEACHA!
Kumbuka NAWAZA tu MKUU!

siKU Njema!
Tutulie na Classic Rumba kutoka kwa KEKELE akidai -DELALI


Au tu Lokassa YA MBONGO amalizie kwa- Marie JOSE

4 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Koero Mkundi 5:40 am  

Kaka Kitururu,

Hakika sikuwezi kwa nahau.
Haya leo umekuja na stili yabmtekenyo sijui kesho utakuja na staili gani?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa 9:55 am  

ukitekenyeka kwa bidii utajamba! pwaaaaaaaaaa

Simon Kitururu 12:42 pm  

@Koero na Kamala: :-)

Yasinta Ngonyani 12:52 pm  

Simon, kweli kazi kwelikweli:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP