Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

NEPI mwanzo na nepi MWISHO!

>> Friday, March 06, 2009

UKIZALIWA unaweza kubahatika kuanza na NEPI au tu lichupi la kanga , shuka au kitenge, kama si linguo tu lililochanwa katika kaptura ya kaka,......

..... katika jitihada za WALEZI kukusitiri TOTO ZURI wakati unajinyea na kujikojole kwa utoto.


Kwa UJANJA na BAHATI unaweza kukwepa kuaga dunia MAPEMA mpaka ikafikia WALEZI kukusitiri kwa NEPI au tu chupi ya kanga, shuka,.... au kitenge , ZEE ZURI usitirike wakati unajinyea na kujikojolea kwa kusahau ya choo kwa uzee.


MAMBO YOTE ni NEPI kulia-nepi KUSHOTO katika dansi hili kama unabahati katika wimbo huu na sebene hili la MAISHA.


TUNAKUMBUSHANA TU na hatutishani!

Swali:
  • AU?
  • Bado unauhakika unataka kuishi sana ?
  • Au unamuogopa Mungu nini ndio maana hutaki kuanza mapema?

Tuendelee na ya CUBA kama CELIA CRUZ adaivyo katika - OYE COMO VA


AU tu CELIA CRUZ amalizie kwa -Azuca Medley

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP