Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika stori TUSIZOZIJUA za BIBLIA za ADAMU na EVA labda ni kweli MKUNGA alikuwa ADAMU wakati EVA ANAJIFUNGUA!:-(

>> Tuesday, June 08, 2010






Kuna ufanyayo TUSIPOFIKIRIA hatuwezi KUSTUKIA unafanya.:-(



Swali:


  • Si unajua ni kawaida kutowaoanisha waheshimiwa na  matatizo ya kujikuta chooni wakati hakuna kitawazio?:-(
  • Si unajua kuna MAPADRE wa kanisa la KIROMANI KATOLIKI ambao tunaweza tusiwe tunajua ni kwanini wanashauri sana kutotumia silaha za kuzui HADIJA asipate mimba kwa kuwa labda wanajua matumizi vizuri yazuiayo HADIJA asipate miba?


Kuna KAZI  mtu AFANYAZO ambazo HUWA HAZIONGELEWI,....
.....na hapa siongelei KAZI zile za  KUSAIDIA shimo fulani la CHOO kujaa.:-(



Na LABDA ndio maana mengi ya ujifunzayo SHULENI HUYASTUKII kwa kuwa darasani  HAYAONGELEWI,...
......na kwa  kuwa  katika MASOMO SHULENI  kunaujifunzacho na kukifanyia mazoezi mwenyewe BILA USIMAMIZI WA MWALIMU labda ndio maana kuna MWANAFUNZI ambaye angalau katika kujifunza kwa bidii mwenyewe MIMBA humjaa.:-(


Swali:

  • SI kuna uwezekano moja ya kazi  ya AMSIKILIZAYE RAIS akihutubia ni kumfanya RAIS  ahutubiaye kujisikia KUNAWANAO MSIKILIZA ingawa wamsikilizao hawakufunzwa kustukia hilo  wakati wamsikilizapo ALOLOMAYE?
  • SI unajua labda moja ya kazi ya walipa kodi wasioijua ni kusababaisha tuwe na MAFISADI ambao  cha kufisadi ni pesa za kodi?


NDIO,...
.... labda moja ya kazi ya MIAKILI yako ni kutufanya siye wengine tujisikie WAJINGA ingawa hujastukia.:-(

LIONE VILE!:-(

NIMEACHA WAZO Mheshimiwa !:-(

Hebu twende UGANDA tujifunze jinsi ya kujitetea OBAMA akitaka kuleta USENGE katika busara zenye kichwa cha habari -EAT DA POO POO



Au tu Jake Benson afanye ujumbe uwe dansabo katika kitu -EAT DA POO POO remix

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Yasinta Ngonyani 8:53 pm  

Duh! haki ya nani kuna kazi Adamu kuwa mkunga mmmhhh! jamani jamani haya.

Simon Kitururu 9:02 pm  

@Da Yasinta: Kama walikuwa Adamu na Eva pekeyao baada ya kufukuzwa bustani ya Eden unafikiri wakati Eva mjamzito ANAUCHUNGU WA KUTOTOA nani alikuwa MKUNGA?

Yasinta Ngonyani 11:30 pm  

Hatuwezi kujua kama Adamu alikuwapo karibu au alimsaidia Eva.:-)

Simon Kitururu 1:16 am  

@Da YASINTA: Ndio maana kwenye TARALILA natunia sana neno :


``LABDA``:-(

o'Wambura Ng'wanambiti! 8:56 am  

@Yasinta: unashangaa nini? Hujawahi kusikia wakunga wa kiume ambao hawakusomea wakiwasaidia wanawake kujifungua ktk daladala?

pengine mt simon ana ukweli wa jambo hili. Hebu mbane uone...lol

Yasinta Ngonyani 12:15 pm  

Je wewe umewahi kumsaidia mama mjamzito kujifungua?

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP