Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Tukiudeku UKAKAMAVU wa uzuri wa NDOTO za kumpata MWAJUMA , usioambatana na MIKAKATI na LENGO la kumpata MWAJUMA!

>> Thursday, June 10, 2010





NDOTO  kwa BAHATI MBAYA zipo,....
.....na  labda NDIO MAANA  kwa bahati NZURI   kila mtu ana mpaka MAJINAMIZI yake .:-(


Swali:

  • AU?

Na ndoto kama MAWAZO tu zipo,...
....na UZURI wa NDOTO kama kilema cha  MAWAZO TU  bila VITENDO  unaweza ukashindwa kumpa mimba mtu kwa kumuota TU au UKASHINDWA HATA  kufanikisha kuwa MWIZI  ingawa kwa NDOTO za wizi hata za magwaguro ya watu WEYE ni  kubwa lao.:-(


Swali:
  • AU?
  • Si unajua kwa kumuota tu  MWAJUMA kuwa ni  MCHUMBA wako haifanyi MWAJUMA ageuke MCHUMBA wako?


Ndio,....
... kunauwezekano NDOTO bila MIKAKATI na LENGO unaweza usitimize ndoto yako ya kuwa MWIZI.:-(


NI WAZO TU HILI na nakutakia kila la kheri  angalau uwe na uhakika wakupata CHOO MHESHIMIWA!

Au ngojea J DILLA atulize kwa kitu- Think Twice




Au tu Q-Tip aendelee kubadili hali ya hewa hapa kijiweni kwa kunyuka mkung'uto - Things U Do

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

o'Wambura Ng'wanambiti! 11:01 am  

duh! leo nimeota ati nakunywa ugimbi karibu na kulewa nkashtuka kabla sijapata stimu vizuri...lol

Yasinta Ngonyani 7:57 pm  

Kaka Chacha Duh! umenikumbusha mie nimeota eti nipo kisiwa cha Madagarscar nikifanya jogging, kushtuka hivi kumbe nipo kitandani......LOL:-)

Anonymous 8:26 pm  

Wanaoutaka uheshimiwa kwa mwaka huu wanaota wapo bungeni,wengine kwa waganga wa kienyeji kupiga ramli.Wengine wanaota wameruhusiwa kuwa MAASKOFU mashoga kwenye nyumba zao za ibada.

Mija Shija Sayi 8:37 pm  

Kitururu hapa umeonge. Bonge la Falsafa.

MARKUS MPANGALA 9:17 pm  

NDOTO IMETIMIA NA LENGO LILIKUWA NA MIKAKATI. wakati mwingine kuiota ndoto ni ubongo kile kitekelezwacho ubongoni. Na sijaota ndoto bali nimetimiza ndoto iliyopangiliwa taralila na katapila la mkaruzo ili kuweka mkeka a.k.a lami. SUBIRI NDOTO ITAWADIA

Simon Kitururu 10:58 am  

@Anony, CHACHA , MARKUS DA MIJA na YASINTA: DUH!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP