Wakati MTO ni ULEULE,....
>> Saturday, June 12, 2010
... unaweza kufikiria maji yaliyopita jana siyo yapitayo LEO,...
...ILA kama ni mfikiriaji unaweza kustukia asilimia kubwa ya MAJI YATUMIWAYO na BINADAMU ni YALEYALE,.....
.... kwa kuwa mzunguko wa maji hapa DUNIANI chini ya anga ni ULEULE.:-(
Kwa hiyo MAJI hata ya MKOJO wa mbuzi ni yaleyale,...
....ambayo yakigeuka mvuke ndiyo yatakayo dondoka kama MVUA ambayo usipoichunguza vianzo VYA MAJI YAKE waweza kufikiria maji yote ya mvua ni masafi kama ulivyo aminishwa kuna BINADAMU anamwili msafi kisa kaoga VILEVILE.:-(
Swali:
- Si unakumbuka mawingu yanaweza kuwa na vumbi au tu hata kemikali za sumu kama tu mabaki ya mikojo mtaroni vilevile hasa ukikumbuka JAPANI baada ya bomu la nyukilia walio kunywa maji ya mvua walizurika kama tu ULAYA walivyowahi kuzurika miaka fulani kutokana na kunyeshewa na maji yaliyoathiriwa na mlipuko wa volkano ya ICELAND enzi hizo vilevile?
- SI unakumbuka KATIKA MZUNGUKO hata udongo uukanyagao labda ni mabaki ya MAITI fulani ambayo miaka fulani marehemu au hata HAYATI chura alioza na kugeuka udongo katika mzunguko ambao leo ni udongo tu VILEVILE?
Ndio,...
... labda maji yaliyokudondokea leo MTONI baadhi ya matone yake ni yaleyale yaliyokudondokea JANA.:-(
Hebu MRISHO MPOTO na MAUNDA walete kitu- Samahani Wanangu
Au tu MRISHO MPOTO na Banana ZORO wanyambulishe kitu katika -NIKIPATA NAULI
Au tu na REMMY ONGALA anyuke tu ndude-PESA
0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment