Chakula cha mawazo-Is U a Ni..er?
>> Friday, August 25, 2006
Mambo ya mfurukuto katika jamii kutokana na tofauti za Rangi,dini,jinsia nk huwa hayanichoshi hata siku moja.Ila haya ni mambo ambayo kila mtu hufikia majibu yake mwenyewe. Au mara nyingi walio wengi hupenda kuuliza tu maswali bila ya kuwa na majibu.Ila majibu ya maswali yetu tukumbuke kuwa ni majibu.Na katika majibu kuna mawili, unaweza ukapatia au ukakosea.Lakini kama binadamu kukosea au kupatia ni njia ambazo hutujenga. Leo ningependa kutoa chakula cha mawazo kwa kuwashirikisha Profesa Kamau Kambon ambaye anaamini inabidi tuwaue Wazungu wote kama moja ya dawa itakayosaidia kuokoa dunia.Cheki hotuba yake hapa.
Profesa Kamau Kambon
Pia bila kumsahau Adolf Hitler ambaye naye alikuwa kafikia jibu kuwa kuwaua watu kama wayahudi, vilema, wasenge, majipsi au waromani na nauhakika watu weusi tungekatiza anga zake angetufyeka zaidi au kisawasawa kama jibu la maswali aliyokuwa akijaribu kutatua.Mcheki hapa akionyesha maringo yake
Adolf Hitler
Ningependa tujaribu kuendelea kutafuta majibu.Watanzania tuendelee kufikiria na tuendelee kujikosoa.
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Umetupa chakula kizito kabisa cha mawazo. Suluhisho la Kamau linarahisisha sana uchambuzi na upembuzi wa chanzo cha matatizo ya watu weusi. Binafsi sidhani kuwa kuna jibu moja la matatizo yetu. Na jibu lenyewe sidhani kama linahitaji umwagaji damu wa halaiki.
Katika kila kundi la watu au wenye rangi sawa, imani sawa au lugha moja hutokea walinzi wa kundi hilo. Mara nyingi huwa ni walinzi waliojiteua na kujipa mamlaka ya kuamulia watu wafanye nini. Utasikia wengine wakisema si ruhusa kuoa mtu wa kabila jingine au dini nyingine. Au wanaweza kuamua tu kwamba pengine watu wa kabila hili au lile ni watu nusu.
Watu wa namna hiyo ‘mafundamentalist’ fulani hawapendi mijadala – wao huanza mjadala na ‘conclusion’ kisha wakafafanua conclusion. Hawaanzi na upelelezi ikesha wakafikia matokeo. Hawawezi kuvumilia mjadala. Wanamiliki ukweli.
Tena husikitika sana pale walio wengi wasipofuata ‘ukweli’ wao. Basi huwa wanakaa kando kando ya jamii wakisubiri sababu ya kudhihirisha ukweli wao. Kwa muda mrefu hufanya mikutano midogo midogo au kugawa vikaratasi vya itikadi.
Ikitokea RPF wanaanza kuvamia Rwanda au wametungua ndege aliyokuwamo mwenzao, au Marekani ifanye jambo dhidi ya nchi yao, au serikali yoyote ipitishe sheria au maamuzi yanayofunga mwenzi wao - ukweli wao hudhihirika. Basi watu wote waliokuwa wakiwadharau hapo mwanzo hujiunga na mafundamentalist. Hawa watu wenye siasa kali hushamiri pale tu matatizo yanapolikumba kundi lao. Watu wote watasikiliza na kuthamini ukweli wao.
Cha kusikitisha ni kwamba – wakati wa amani - kwa sababu mbalimbali watu wanaofikiri tofauti na mafundamentalist huwa wanaogopa kuwapinga vile wataonekana dhaifu hata kama machale yanawatuma vyengine. Wanaogopa kuonekana wameasi kabila au kundi. Wanaogopa kuonekana labda wao si waafrika sana au wajeremani sana.
Katika historia ya zama hizi hakuna aliyefanikiwa kufanya mauaji ya halaiki na kutokomeza kabila zima la watu ikesha akaishi raha mustarehe. Hakuna alnayefanya udhalimu na kuishi kwa amani milele.
Nakubaliana sana Mwandani na Ndesanjo.Mwandani kuhusu kuwa hawa jamaa wanaanza mjadala na conclusion nilikuwa sijawahi kufikiria hivyo.Asante kwa kunipa angle hiyo ya mtazamo
Post a Comment