Usenge na Ubasha ndani ya Tanzania ni Vitendo vya uvunja sheria lakini.....!
>> Monday, August 14, 2006
Siku hizi hasa jinsi teknolojia inavyonifanya nijikute sina maneno ya kiswahili ya mambo mengi, huwa ninajiuliza maswali kuwa imekuwaje kwa kiswahili tumeweza kuwa na maneno hata ya kutofautisha wanaopenda kulawitiwa na wale wanaolawiti wenzao. Nakumbuka kuna kipindi nilikatisha mitaa ya pwani na kusikia kabisa mtu akisifiwa kuwa yeye ni basha, lakini hapo hapo msenge huonekana hafai kuishi.Mimi huwa najiuliza inawezekanaje Basha akawepo pasipo na msenge? Sasa naona Tanzania tumepata na kesi ambazo zilivuma duniani za Mapadre au maaskofu kulawiti watoto wa watu wakiume. Soma hapa ujionee.
Chakusikitisha ni kwamba bado Tanzania watu hatuzijui sheria zetu zitulindazo.Ingekuwa Watu wangezijua sheria kama zijulikanavyo zile za uasherati basi ingesaidia hata kuondoa rushwa nchini.
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Kwa hiyo Fr. Sixtus alikuwa na uhusiano wa Ki-ngono Kwa Takriban kipindi cha miaka 2.
Ni wazi Kwamba Basi Mlawitiwa alikuwa ni mtoto wa miaka 15 wakati walipoanza hako kamchezo kao. Huu ni unajisi na hata nchi zinazoruhusi ushoga kisheria, watoto chini ya umri unaokubaliwa, hawana ridhaa ya kufanya mapenzi hata kama wanafanya hivyo kwa makubaliano. Mtu mzima hapa lazima utaubeba msalaba lakini sio kwa nondo 30 alizopewa huyu msoma misa.
Lengo la sheria za nchi siku zote zilinge zaidi kuwakinga wadhaifu katika jamii, i.e, watoto, wazee, walemavu, wasio na ajira etc.
Unasikitisha hasa zaidi mtu aliyekwenye nafasi ya kuaminiwa katika jamii k.m. kasisi, mwalimu, au Daktari anapoamua kutumia wadhifa wake kujinufaisha.
Ili kuepukana na haya, Jamii inatakiwa kukua na kwenda na wakati, muda umefika ambapo uhusiano wa HIARI kati ya watu wazima wa jinsia moja uruhusiwe kisheria. k.m mtu zaidi ya miaka 18 awe na uwezo wa kuchagua kama atakuwa na mpenzi wa jinsia yake au ile ya upande wa pili.
Hii itaondosha, tabia ya watu kuwanyatia watoto wetu, kwasababu wataweza kuchagua kuwa katika uhusiano wa wazi na bila hofu ya kushtakiwa au walu kufungwa.
Kinachofanyika ndani ya chumba baina ya wawili wapendanao hayatuhusu ili mradi wamekubaliana kwa moyo mmmoja. Kama hawahatarishi maisha yetu au yao, Hawaharibu mali zetu au za umma, na hawatukoseshi usingizi sasa nini tena tuwafuate-fuate?? Kila mtu achague jinsi anataka kujistarehesha Bwana, Maisha ni mafupi na tusiwaamrie watu wengine jinsi wanatakiwa kujistarehesha.
Watu hawa tunawaita mashoga, jamii inawazonga na hali, wengi wao ni wachapa kazi vibaya mno, wanalipa kodi na wanatunza sheria zooote za nchi. kwanini basi suala ambalo ni la kimaumbile na si kwa kuchagua liwe kigezo cha manyanyaso?? Ni kwasababu kama hii basi tumewapoteza ndugu zetu hata wenye uwezo wa hali juu kwenye fani mbalimbali kama Kiiza Kahama etc.
Haya basi, Padre huyu amepatikana na hatia, hukumu miaka 30!! Ee Mungu, nafikiri hapa Jaji kaamua kumporomoshea nguvu ya sheria kwa kishindo. Miaka 2 au 3, ingefaa, ikiwezo pia uwezekano wa 'Parole'. Zaidi ya yote, Padre huyu angetakiwa kufuata mafunzo ya Ngono, jinsia na jinsi ya kukabili shauku zake.
Tunaomba tamko la Askofu kuhusu suala zima kwasababu, ukichia mbali yote haya, Padre wake aliapa siku ya upadirisho kubakia mkiwa i.e bila mwenzi ya ndoa au kufanya shughuli zozote zenye mwelekeo wa kingono-ngono.
Naamini jamii haikubali kujadili suala hili, lakini kumbukeni, kukataa hakumaanishi kwamba nd'o mwisho, hili litabakia kwenye anga la giza lakini kukicha tutakumbana na mengi ya usiku ul'opita yakihitaji usuluisho wetu. Polisi wetu, Mahakama zetu, Jela zetu, wanasheria wetu, vyombo vya Habari, zielekeze nguvu zake katika matatizo mengine makuu yakulijega taifa letu.
Tuondoshe sheria za kibaguzi, kumbagua mtu shoga ni Ubaguzi kama ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, unagusa suala la Haki za Binadamu.
Post a Comment