Mmecheki Darwin's Nightmare?
>> Saturday, August 12, 2006
Nimepata link za documetary hii kutoka kwa washikaji . Kongoli hapa. Ukifika hapo utapata kuzipata sehemu zote za filamu hii.Iliozaa habari ifuatayo kwenye Nipashe.
2006-08-12 09:53:52
Na Namsembaeli Mduma, Dodoma
Wabunge wa Bunge la Muungano, wameiomba serikali iwakamate washiriki wote waliohusika kutengeneza au kufanikisha filamu ya The Darwin’s Nightmare(Jinamizi la Darwin), maarufu kama filamu ya mapanki, kufuatia uongo walioutumia katika sinema hiyo kuichafua sura ya Tanzania nje, pamoja na kuwadhalilisha Watanzania.
Aidha, imeombwa iwachukulie hatua kali za kisheria Watanzania wasaliti hao, pamoja na wahusika wengine, badala ya karipio tu, ili wawe mfano kwa wote wenye nia au watakaojaribu kufanya udhalilishaji kama huo ulioonyeshwa kwenye filamu hiyo, mara baada ya uchunguzi unaoendelea juu yao kukamilika.
Sambamba na maombi hayo, wabunge hao, bila kujali ni wa upinzani au chama tawala, wameitaka serikali iandae filamu mbadala itakayoonyesha uwongo uliotumiwa kwenye hiyo ya The Nightmare, ili kuuonyesha ulimwengu ukweli kuhusu Ziwa Victoria na biashara yake ya sangara, kwa kuwa asilimia kubwa ya yaliyozungumzwa ni uzushi.
Lengo jingine lililotajwa ni kuisafisha Tanzania kwa ujumla kuhusiana na kashfa hiyo nzito ya silaha, inayoelezwa kulenga kuiharibia nchi kwa mataifa mengine juu ya amani iliyoigubika.
Hoja hiyo ya kutengenezwa filamu mbadala, licha ya kuungwa mkono na wabunge karibu wote wa Bunge hilo, iliwasilishwa kwanza na Bungeni hapo jana asubuhi na Kambi ya Upinzania kupitia Msemaji Mkuu wao, Bw. Khalifa Suleiman Khalifa.
Aliungwa mkono kwa karibu na Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA).
Vile vile, hoja ya kutengenezwa filamu hiyo nyingine ya kweli ilisemwa Bungeni hapa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Bw. Johnson Mwanyika, wakati akisoma azimio la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuhusu filamu hiyo yenye utata.
* SOURCE: Nipashe
Cheki mwenyewe.
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Ahsante Custo, nimedownload hivyo viungo hivi sasa naangalia bila wasi.
Post a Comment