Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Kitendawili?Tega. Kuna Nchi inayojidanganya kuwa ina amani na umoja.....Jibu ni ...

>> Friday, August 25, 2006

Sehemu zote nilizotembea utaambiwa Watanzania ni tofauti. Ni wapenda amani na wana umoja na sifa kemukemu hasa ukilinganisha na wananchi wa nchi nyingine za kiafrika.Utaambiwa Tanzania ni nchi yenye umoja na amani. Unaweza ukaamini kuwa ni ukweli, mpaka uanze kujichanganya kwenye jamii ya Kitanzania ndio utastukia kuwa mambo mengi ambayo yana sadikika kuwa yamekufa bado yananawili na yapo tu katika uvuguvugu ambao kirahisi tu yanaweza kulipuka.Utagundua Watanzania hawapendani.Husengenyana na kutaka kuvutana chini kama kawaida tu.

Kuna mambo mengi ambayo unaweza kuyapa uzito lakini kubwa ambalo linaweza kutoa kasheshe kirahisi Tanzania ni la udini. Hasa, ni vigumu kukana kuwa bado kuna vichokochoko vinaendelea kati ya Uislamu na Ukristo ndani ya Watanzania.Kama wewe ni mtu usomaye mablogu ya Watanzania utagundua hakuna habari itakayo changiwa na wengi kuliko inayo husu maswala ya dini hizi mbili. Mtu tu akithubutu kusema hoja yake ambayo inagusia swala la udini na linaloonyesha kuegemea katika dini moja basi lazima iwe kasheshe. Cha ajabu ni kwamba majadiliano mengi ya maswala ya dini humu katika Mablogu ya Watanzania hujaa matusi mpaka utaanza kujiuliza, hivi si ni kweli kuwa dini zote hizi mbili zinakataa maswala ya matusi?

Chakusikitisha ni kwamba asilimia kubwa ya Watanzania kwa mtazamo wengi, wana majina tu ya Kikristo au Kiislamu, lakini ni wachache tu ambao wanaweza kusema kuwa ni wanadini asilimia mia.Hapa nawaachilia mbali wale waliokuwa na bahati ya kuwa na majina ya asili ya Kitanzania wenye dini za asili. Lakini pamoja na kutofuata kikamilifu mafunzo ya Mtume na Yesu, ni rahisi kwa Watanzania kutukanana hata kupigana katika jina la dini hizi ambazo hata kutimiza sheria zake hawatimizi.Sasa ni nchi ya amani gani kama ina watu ambao wanaweza kupigana na kutukanana bila mpango? Kwa sababu kama unaweza kupigania kitu ambacho hata uhusiano wako nacho ni hafifu mimi naona ni vita isiyo na mpango.Siamini kuwa hata uko mbinguni utakwenda. Naamini kabisa kama ari hizi za kutetea dini tungekuwanazo hata katika kutetea haki zetu na hata kujenga nchi, tungekuwa mbali. Hivi Raisi JK kawapa kazi zenye wadhifa waislamu wangapi?Ni moja tu maswali yaulizwayo na hili litakuonyesha kuwa dini yako inakuweka katika kitengo fulani na kwamba udini bado unanguvu sana Tanzania.

Tanzania bado kuna ukabila sana tu. Dalili zake ni nyingi.Moja yapo ya dalili ni jinsi watu wanavyopenda kuchunguza nani anaajiriwa na kama anatokea kwenye kabila la bosi. Na ni kweli watu bado hupeana kazi kikabila, pamoja na mambo mengi tu. Sasa ni nchi gani ambayo ni ya amani yenye watu wamakabila yaliyochanganyika kila mkoa ambayo inaendeleza ukabila?Kwa maana hili ni jambo ambalo linaletamchafuko wa amani kirahisi kabisa.

Huko kwenye umasikini na kukosa elimu ndio usiseme. Kwa kukosa elimu sizungumzii kama ni kwenda shule tu. Maana mimi naamini kuwa unaweza kuwa umekwenda shule lakini ukawa hujaelimika. Umasikini unasababisha ukosaji wa amani. Unawezaje kusema kuwa nchi ina amani wakati kila mtu aliyepata kidogo anajenga fensi kuzunguka nyumba yake. Nchi yenye masikini wengi wasio shiba vizuri si nchi ya amani.Sijawahi kusikia mtu mwenye njaa akawa na amani hata rohoni mwake.Sasa mtu huyu hawezi akawa anachangia kuweka nchi iwe ya amani.Nchi si kitu bila watu. Na nchi yetu kama haitaweka misingi ya kuwa na wananchi walioelimika haiwezi ikawa ya amani. Maana mafanatiki wengi ni watu ambao wana zugwa kirahisi na mtu wanayemuamini bila kufikiri au kuwa na nguzo za kumuezesha kupata majibu binafsi. Raia walioelimika ndio pekee ambao wanaweza kufikiria na sio kufuata tu mambo na kuanza kuchinjana.Raia hawa watakuwa nauwezo wakuona picha kubwa na hatima ya hatua zao katika jamii na kwao binafsi.Mpaka sasa hivi elimu ya Tanzania kwa kiasi kikubwa haimuelimishi Mtanzania.Inamsaidia kupata digrii na ikiwezekana asilimiakubwa akiwa amekariri masomo. Hivyo siwezi kuiita nchi kuwa ina amani ikiwa elimu ambayo bado inatupa haituwezeshi kutujenga kujitatulia matatizo yetu binafsi na ya kijamii.Mfano haituwezeshi kujiajiri.

Nirahisi kuandika mambo mengi lakini bado naamini haya mambo manne tu, udini , ukabila, umasikini na kutokuelimika kumenifanya ni amini kuwa Tanzania amani tunayodai tunayo si ya kweli. Kinachofanya tujiamini tuna amani ni kutokana na kuzungukwa na nchi zilizoko ndani ya vita kabisa. Naomba tusijisahau na kudhani kuwa siye tumesalimika.Na vita ikitokea bongo itakuwa mbaya kuliko zote .Kwanza tumechanganyika.Mtaa mmoja makabila kibao halafu achilia mbali dini.Mungu ibariki Tanzania.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP