Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Je Waafrika tumeathiriwa na Stockholm Syndrome?

>> Friday, August 25, 2006

Kama vyombo vya habari havitudanganyi, basi ni kweli kuwa, katika makundi ya watu ambao wanawapenda watu wanaowanyonya na kuwaonea, Waafrika wanaongoza. Kuna hali ya kisaikolojia ambayo inajulikana kama Stockholm Syndrome ambayo inasababisha watu ambao wako kwenye kibano wawapende na kuchagua kuwa upande wa watu wanaowapa kibano.Hali hii ilipata jina kutokana kitendo kilichotokea hapo Norrmalmstorg, Stockholm , ambapo majambazi yalichukua mateka wafanyakazi wa benki. Pamoja na amjambazi kuwa ni ya hatari wale mateka wafanyakazi wakawazimia majambazi. Badala ya kutaka kujiokoa, wakawa wanawasaidia na kuwatetea majambazi hata walivyobaini kuwa wangeweza kuwatosa majambazi na kujiokoa. Kwa mtazamo wangu wa kila siku hii ndio hali ambayo bara zima la Afrika inalo. Tofauti ni kwamba nchi gani imechagua nchi za kiarabu na nchi zipi zimechagua nchi ziongozwazo na waulaya,marekani nk.Au unaweza ukaiangalia kuwa hawa majambazi ni kama hawa viongozi wetu Afrika ambao kwangu mimi ni sawa tu na hawa wageni ambao wanajinoma kutunyonya na kutudhalilisha.









Waswidi ambao walitekwa kwenye banki lakini badala ya kuwachukia majambazi wakawa wanawahusudu.










Pamoja na kujua kabisa kuwa tunanyonywa na nchi za nje, bado hupendelea mahusiano hayo kuliko kutetea kujijenga na kutengeneza mazingira ambayo tunaweza kucheza mchezo sawa na hawa wanyonyaji.Na kama hatuamki wenyewe hakuna hata haja ya kuwalaumu hawa watu kwa kujinoma katika kutunyonya. Huwezi kuamini eti mpaka leo Nigeria inaagizia nje mafuta yaliyosafishwa(refined), wakati yenyewe ndio nchi ya Afrika iongozayo katika kuuza mafuta ghafi nje.Huwezi kuamini mpaka leo asilimia karibu zote za mali ziuzwazo nje kutoka Tanzania huwa ni mali ghafi.Na si siri kuwa wote tunajua mali ghafi haina thamani kama bidhaa iliyo kamilika. Tanzania ukiachilia sangara ambao angalau wahindi pale ziwa victoria wanalipwa huwezi kusema kuna mali nyingine ambayo ni asilimia miamoja inatoka kama bidhaa iliyo kamilika.Sijui labda maua. Na kama sikoseiwafanyakazi wanaofanya kazi katika viwanda vya samaki Mwanza huwa hawana mishahara mizuri pamoja na kuwa mashirika yao hulipwa vizuri.Unaambiwa ni Botswana peke yake ambayo serikali inalipwa ipaswavyo na inaelekeza pesa kwa wananchi ipaswavyo Afrika.
Narudia, nadhani sisi Waafrika tuna Kastockholm Syndrome. Kama tusingekuwa nako, na kama ni kweli maisha ni magumu Afrika kuliko sehemu yeyote duniani je kwanini ni Waarabu wanaongoza kujilipua mabomu katika kudai haki zao?. Sawa utasema ni maswala ya udini. Kuwa ukijiua unapata tiketi ya first class kwenda mbinguni ambako kuna unono kibao, na kama mwanaume utapata mademu kibao mbinguni. Sasa utasemaje kuhusu Kamikaze Pilots wa Japan ambao walikuwa wanajiua kutetea nchi yao. Vile vile usisahau akina Tamil Tigers .Chini ya The Liberation Tigers of Tamil Eelam hawa watu wako tayari kufa nawe ukiingilia angazao. Hakuna cha kusema kuna mbinguni wala nini.









Mapailoti wa Kijapani wa Kamikaze









Bado naifikiria siku ambayo Waafrika watagundua adui yao na kupambana kama waarabu wajilipuao , watamil au hata mapilot wakijapani. Silaha za muafrika ni nyingi. Lakini fikiria ikiwa SILAHA KUBWA KULIKOZOTE KATIKA VITA HII ZIWE NI UMASIKINI, UJINGA NA MAGONJWA! Waafrika kila siku tunaongelewa katika kila televisheni duniani kwa umasikini wetu, ujinga wetu na magonjwa yetu . Sasa tukaamua haya mambo matatu ndio silaha. Kwanza kutokana na umasikini, itu halalishie kuwa hakuna mpango kuishi, lakini katika kujiua tunakufa nao mwanyonyaji wetu wanaotudhulumu. Kama wajinga basi hatujui thamani ya maisha yetu, lakini katika kufa tunakufa na wanyonyaji zetuwanao tudhulumu.Halafu kunakaukweli kuwa hatuthamini maisha yetu Afrika , kumbuka askari wanavyo tupiga marungu kila wakati. Kama wagonjwa basi tunajua kabisa tayari tuna kufa hivyo tuna chagua kufa na wanao tunyonya. Naamini hakuna nchi duniani haitataka kusaidi kutatua matatizo yetu Afrika baada ya muda mfupi tu tukianza kujiuanao. Na kwa maswala ya magonjwa hatuitaji hata kujilipua maana magonjwa tusifiwayo nayo Afrika nafikiri yana makali ya usuisado bomu kabisa.









Mwanamama Wakiarabu akiwandani ya fani




Naombea siku hii isifike!Naombea tuwezekuchukulia matatizo yetu kama changamoto ya kutuwezesha kugundua njia zetu wenyewe zakutatua matatizo yetu! Lakini najua ukimsakama mjusi sana hugeuka nyoka. Bado na kumbuka ile Tanzania bikira iliyouwa na matumaini angavu iliyosakamwa mpaka sasa imegeuka kuwa Tanzania ya majambazi, walarushwa, malaya nk.Lakini bado nina imani na Tanzania.Mungu ibariki Tanzania! Mungu ibariki Afrika!

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP