Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUJIFUNZA KUNYA . Samahani! KUJIFUNZA kwenda HAJA KUBWA!

>> Saturday, November 03, 2007

Swali:

  • Ushawahi kuona mtoto analia kwa kushindwa kuamua anyonye au anye?
Kujifunza, unaweza hata kabla hujajua kuwa hujui.

Lakini....
....ukikiri moyoni kuwa hujui, unaongeza asilimia za kuwa mjuaji.

Tatizo ni kwamba, ukijifanya mjuaji utakufa hujui kuwa muuza maembe mnashea kashata.

DUH!

Kunya si kitendo rahisi.
Ndio maana unaguna wakati ukistarehe chooni au pale ulipoenda kuchimba mzizi.

Kunya ni starehe......
....kwasababu ni ushahidi kuwa umekula.

Staili za kwenda haja kubwa, mara nyingi hutegemea unapolengesha kitita kidondokee.

Unaweza kukaa au kuchuchumaa, kama kidondoko si mharisho.
Kwa sababu mkao wa kuharisha karibu kila mkao unakubali.

Swali:
  • Wakati unataka au kunuia kufanikiwa, umestukia kuwa unalenga sehemu fulani kama tu shabaha za chooni?
  • Lakini kama wewe unabahati, si mkao wowote tu ambao huufikirii unalenga tu katika goli la kuwini?

DUH!

Tatizo wenye bahati hatuko wengi :-(

DUH!
Naacha!
Tulia na Lady Jaydee akikupa Siku Hazigandi

2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 2:16 pm  

Hahahahha! Wewe nawe wakati mwingine ha-ha!

Simon Kitururu 2:44 pm  

@Dinah:Si unajua tena siku nyingine mawazoni vitu vinakaa kushoto:-)

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP