Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UMECHEKI BONGE LA PAJA?Ngojea nijivunge lakini....!

>> Friday, November 02, 2007

  • Katika nyama ya kuku , wengine hupendelea firigisi.

Ila...

......katika tamaduni na mila fulani fulani hatakama unapenda paja ,ukikaribishwa firigisi ni mwiko kuikataa.Chochote ukaribishwacho ni mwiko kukataa angalau kuonja.

Kama mstaarabu, waweza kulazimika kukaa kimya au kusifia pia paja kwa kuepuka kukiri unapendelea firigisi kwa kuogopa kuonekana wewe mtu mbaya.

Uwezo wa mtu kuvumilia asiyopenda kwa kukwepa kuonekana mtu mbaya, ni mkubwa sana.
Mtu usipoangalia unaweza kukaishi maisha yako yote unajaribu upendeke.

Hebu msikilize Alpacino akizungumzia Mtu Mbaya ndani ya sinema Scarface.(ONYO:Anatumia lugha mbaya ambayo baadhi wanaweza kutafsiri kana kwamba anatukana)


Naamini , kuogopa kuchukuliwa vibaya kunasababisha ambao wameshachukuliwa vibaya waendelee kunyoshewa vidole kinafiki kuwa ni wabaya na ambao ni wabaya.

Swali:

  • Kama unapenda firigisi, ni mara ngapi umelazimika kuonja paja?

Uzuri wa swala ni kwamba, paja kama ni chakula, ukishikwa na njaa na kulila hufi. Njaa ikiwa kali nguvu ya uchaguzi hupungua, ukianza kushiba ndio utakumbuka zaidi kuwa wewe ni mtu wa firigisi.

DUH!

Baadaye basi!
Tulia na Massive Attack na Tricky wakija na Karmacoma


Baadhi ya picha zangu na wadau ambao hawajanitenga bado...:-)

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP