Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

UKISTUKIA umekanyaga MAVI. Samahani! KINYESI.

>> Wednesday, October 31, 2007

Katika pitapita za kuendeleza libeneke, unaweza ukastukia umedakwa na harufu mbaya.
Wengi wetu hatuhusudu harufu mbaya na hatukawii kukiri hilo kwa nguvu zote!

Cha ajabu....

.. asilimia kubwa ya wakimbiao kitu au harufu mbaya, hujistukia wamegeuka kujaribu kucheki ni wapi harufu mbaya inatokea.

Swali:

  • Ukisikia kijambo, haujawahi kutaka kujua ni nani kajamba?
Sasaaaa......

Baada ya kushuhudia ni mzoga gani unatoa harufu na kuona yale mafunza yakifurahia kitoweo , hapo ndio binadamu huendeleza madoido, kama vile ya kutema mate , kubana pua , kujipepea na kadhalika kadhaa.Unaweza mpaka kumshangaa kwanini mdau alijaribu kukitafuta hata kwa macho tu hicho kitu kitoacho harufu kama kinamchefua namna hiyo.

Lakini....

.... wadau wabanao pua na kutema mate kwa sana wastukiapo kitu kichefuacho roho , ni wakali wa kukausha wakijamba kwa bahati mbaya hadharani au pale waachiapo ushuzi chobisi wakitarajia hakuna atakayetokea mida hiyo.

DUH!

Swali:
  • Ushastukia ukikanyaga kinyesi kikutiacho kinyaa, baadaye unaweza ukakishika kwa kisingizio cha kusafisha viatu?
  • Au ulifikiri ulipoburuza viatu mchangani na pale kwenye majani vimavimavi viliondoka vyote?
DUH!
Naacha !

Tulia na RICHIE STEPHENS na COCOA TEA

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Mija Shija Sayi 1:17 pm  

Kitururu mazungumzo yako huwa nayafananisha sana na Mazungumzo baada ya habari ya RTD.

Kazi nzuri kaka.

Anonymous 4:56 pm  

Kaka hapa naona unawagusa watu flani ambao huwa wanajiona wapo right all the time, yani hawezi kuharibu sasa wanapoharibu ,hapo ndo drama utaona madoido sio polepole!

Safi kaka
Endeleza kazi nzuri.

Egidio Ndabagoye 7:44 am  

Duh! Si utani ishatokea sana

Anonymous 11:52 pm  

:)

Simon Kitururu 2:19 pm  

@Wote!Asanteni kwa kunipitia hapa chobisi!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP