Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KATIKA kukwepa HALI HALISI igusayo MAISHA YETU!

>> Wednesday, October 10, 2007

Hali halisi haiwezekani ikawa na utamu tu bila chachu pembeni yake.

Hali halisi, wakati inakupa utamu dakika hii , inaweza ikawa inakukumbusha ni nini kitafuata baada ya utamu, ambacho kinaweza kikawa ni utamu zaidi au ikawa ni kukukumbusha kuwa kutokana na utamu huu uupatao sasa , ushaharibu kesho au nusu saa ijayo.


Sisi watu, hujitahidi kukwepa hali halisi, nakuiwekea mipaka izungukayo hali tuzipendazo tu.
Tunapenda fenesi lakini sio mbegu zake.

Katika kukwepa hali halisi ya dunia...

  • Matajiri...
... wanajifanya hawaoni maskini. Ni rahisi hata kujirungushia ukuta katika nyumba yako ili hao maskini wakae huko huko nje.

  • Wanadini kama Marasta, Walokole, Wabwiti, Wakristo , wa.....nk...
....wengi wao wanakwepa hali halisi kwa kutuambia wamegundua ukweli , ilikujilinda ndani ya huo watuambiao kuwa ni ukweli, ili wengine wote wasije leta za kuleta na kusababisha hali halisi wanayojiaminisha nayo, iwe ngumu zaidi kueleweka.

Swali:
  • Umefanikiwa kuweza kusababisha watu wengine wasijue hali halisi yako kwa jinsi ulivyokwepa hali halisi leo?


Hali halisi nishai!

Ndio maana watu tunajifanya tunamsikitikia marehemu ili kuja kula ubwabwa msibani, kutokana na kushindwa kusema hatuna msosi nyumbani.

Kukwepa hali halisi , ni sanaa kali!

Inaweza kukufanya uonekane bomba la mchekeshaji ,kumbe unaficha tu huzuni iliyokujaa moyoni.

Hukawii kumsifia demu au bwana yako , kuwa ni mzuri kubwa kuliko, wakati unajua watu wengine wote wanakujua kuwa unamuona hawala yako ndio bomba zaidi.(Si ndio maana ukawa na wapembeni?)

Kukwepa hali halisi si mdhaa!

Inaweza ikakufanya ushinde baa na na kupigana na wanaume wenzako ,kumbe ni kwa sababu unapigwa na mke wako nyumbani.

Inaweza ikakufanya usifike kwa manukato na kunukia vizuri, kumbe ni kwa sababu tu unakidonda ndugu kunako.

Unaweza kuokoka, kumbe kwasababu umechacha tu. Si unajua maisha ya kilokole yanasemekana gharama zake ni za chini kidogo?

Swali:
  • Ushastukia msemo wa serikali yetu wa kwamba ;uchumi umepaa, ni sanaa ya kukwepa hali halisi?


Lakini ....

Yote ni maisha!

Si unajua tena!...
.... kama kila mtu angejua hali halisi yako, ingekuwa usumbufu pia.

Si unajua tena....



  • Jamaa wakijua unazo, utakopwa mpaka ukome?AU?

  • Jamaa wakijua umechacha, wengi ambao mara nyingi ndio wajitangazao kuwa marafiki zako , watakukimbia

  • Jamaa wakijua unamdudu , kuna anga wataanza kukukwepa , ingawa wanajua huwaambukizi.

Swali:
  • Unaamini viongozi wetu walivyopima Mdudu juzijuzi kisiasa, wakiongozwa na Raisi wetu Kikwete , wote matokeo yao yalikuwa safi kama matokeo ya Kikwete?

  • Hali halisi yako ikoje? (Na maanisha , ukipima Mdudu ukajikuta unao, utatutangazia?)
  • Hali halisi yako ikoje?( Na maanisha, unaogopa kupima UKIMWI eeh?)

Lakini .....

Kitu kizuri katika maswala ya hali halisi,.....
......... hakuna ambaye anajua hali halisi ya mwenzake, hata kama wako wengi wajifanyao wanajua ya wenzao.


Naamini kila mtu anajua hali halisi aliyo kuwa nayo ki binafsi.
AU?


Na...
......Mchezo huu tushirikiyo, wa kujaribu kukwepa hali halisi, ndio unaitwa
MAISHA.

AU?

Nakutakia kila la KHERI katika KUJARIBU kukwepa au kutufanya tusijue HALI HALISI yako!


--------------------------------------------------------------------------------------------
Ngoja nikuache na picha fulani nililizozidaka hivi karibuni....


Picha za baadhi ya waliohudhuria Mkutano wa Watanzania, siku kadhaa zilizopita ....



DUH!
PATRA yuko kichwani na wimbo wake wa longi hizoooo... Msikilize kidogo kabla hujaendelea...


Picha za Shughuli ya COBRA

Naanza na Cobra mwenyewe

..

Cobra Vibes


Picha nyinginezo ndani ya Party ya Cobra:

Bobby Culture , Super ONE , Simon .....



Mzee wa A-Town aka Musical Blak


BONANZA the GREAT! Samahani nilikutenga kiwanja....!
Tuko Pamoja lakini!


Kikao cha Kwa Raymond aka MKUU wa KIKAO!

Naanza na MKUU wa KIKAO..

Ngojea CHACHA atuambie...!




Baadhi ya niliyowadaka kwa Mkuu WA KIKAO...



Hebu Ronaldo atukumbushe ile miondoko ...


Kwa wadau ambao sijaingiza picha, TUKO PAMOJA! Nimeziingiza haraka haraka na , hii kitu mara nyingine haina Baraka.
Hapa tu wakati naandika nimemkumbuka Mzee DEO!
Tumalizie na enzi hizo hizo...
Unamkumbuka MC Hammer?

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP