Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

HAKUNA JIPYA, yote yako MUKICHWA!

>> Friday, October 05, 2007

Pamoja na yote..

Binadamu tunaamsha tu yaliyoko ubongoni.Tunajaribu kufanya yaliyo ndotoni , mawazoni, yaonekane mbele ya macho yetu!Ukionacho mbele yako, ambacho binadamu mwingine amefanya, inawezekana ikawa ni jinsi alivyokosea kukitoa ubongoni au mawazoni na kukiwasilisha duniani.

Machache binadamu kafanikiwa kuyatoa ubongoni na yakawa kitu halisi ulingoni.
Ni machache zaidi binadamu aliyofanikiwa kuyatoa ubongoni na kuyaweka kama alivyoyaona ndotoni au katika kimbunga cha ubongo(brain storm)

Swali:

  • Si ushawahi kutoridhika na ladha ya togwa baada ya kuionja na kustukia haifanani na ilivyokuwa mawazoni mwako kabla ya kuionja?
Si ushawahi kustukia!
Mtu aliyevaa nguo, anaweza aasionekane kama jicho la ubongo lilivyokustua ndio maumbile yake yalivyo, baada ya kumchungulia akiwa bila nguo.

Duh!

Lakini sisi binadamu....

....tunajaribu kufanya yaliyo ubongoni, ndotoni, mawazoni ,ili yawe mbele ya macho yetu , ladha zetu nk.

Tunatofautiana tu, katika ujanja wa kuyatoa mukichwa , nia na umuhimu wa kuhangaikia kuyaleta yale tuyawazayo, tuyawezayo; yaonekane , yahisiwe au kubadili kitu fulani kama tukionavyo kwenye jicho la ubongo, kijiweni.

Swali:
  • Unakumbuka mambo yote yatokeayo ndani ya ndoto uziotazo?
  • Mangapi yaliyotokea kwenye ndoto zako, ulishawahi kuyashuhudia, kuyasikia au kuyatenda, kabla hayajajitokeza kwenye ndoto zako?
  • Hivi , unakumbuka de javue?

Mengi tuyaonayo, ambayo ni matokeo ya utundu wa binadamu , ni mrahisisho wa yale mambo ambayo yalionwa na jicho la ubongo la binadamu.Tunarahisisha yaliyo ubongoni kutokana na kutojua jinsi ya kufanya yote yaliyo ubongoni yawe ndio hali halisi kirahisi.Unajua, binadamu kwa asili ni mvivu.


Kumbuka hata majinamizi(ndoto mbaya) ukiyaamini , ni hali halisi. Ni kitu halisi kikuzinguacho na kukukosesha usingizi, kitu ambacho nikikuona kesho yake nitashuhudia hali halisi yako wewe baada ya kukosa usingizi.
AU?

Swali:
  • Wenye imani , si ndio wanakuambia, imani yako ndio itakayokuponya?

Nikirudi kwenye hoja...

Tuvionavyo sasa hivi si jambo jipya zaidi ya yale yale yaliyomo ndani ya vichwa vya watu hata kama hatuvistukii.

Tatizo mojawapo la ubinadamu , ni kutostukia baadhi ya mambo yaliyomo ubongoni mwetu.

Swali:
  • Ushawahi kuingia katika mtihani ukiamini hujui utafanyaje kutokana na kutojiandaa vizuri , halafu mtihani ukawekwa mbele yako , ukaona maswali na kuanza kushuka pointi mpaka unajistukia; kumbe nalijua swala?


Tatizo jingine la ubinadamu ni kuambukizana mitazamo na jinsi ya kutafsiri ya dunia.

MITAZAMO ya WAJANJA na TAFSIRI ZA YA DUNIA za WAJANJA , ndio binadamu wengine wanashikilia kuwa ni ukweli, MPAKA ATOKEE MJANJA MWINGINE mwenye mtazamo na uwakilishaji wa tafsiri ambao watu wengine wengi wanashindwa kuubishia.

Ushastukia !

Dunia ya leo iendeshwavyo kwa mafuta, karibu kila mjanja anajua imeharibu mazingira ya dunia na kushindwa kumuongezea binadamu raha wala furaha.Ila wajanja waliotupeleka katika njia hii bado ndio wameshikilia dunia.

Swali:
  • Unafikiri mababu zetu wa kale walikuwa hawali maisha ingawa hawakujua gorofa wala baiskeli?
  • Au, unafikiri , technology na maisha yaaminikayo kama bomba leo ni timilifu?
  • Au unasubiri mambo yatimilike ukifika mbinguni?

DUH!
Naacha!

Siku na Wiki Mwisho Njema!

Nakuacha na EVERLAST , wakija na kibao YESU MWEUSI.

0 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP