Binadamu Akicheza Muziki, hustukii KAKICHAA kiduchu?
>> Tuesday, October 30, 2007
Moja kati ya mahusiano kibao binadamu aliyojikutanayo au kujitafutia, ni uhusiano wake na muziki.
Jaribu kumuangalia binadamu achezaye mziki, halafu wakati anaendelea kusakata ngoma, mtazame tu huku umefuta sauti ya mziki.
Anachekesha eeh?
Napenda sana mziki, lakini ushafikiria ni nini kinakufanya utikise mguu ukinogewa na wimbo wa wa Kabasele ya Mpanya?
Miziki kiboko, kuna mingine kama ya kwenye makanisa fulani ya watu waughaibuni, inabidi uimbe au usikilize huku unaonyesha sura ya upole kana kwamba unapata utukufu.
Halafu kuna ile miziki ambayo ikipigwa, wajanja wakagundua kuwa staili nzuri ili wewe usifike unajua kucheza , ni lazima umkatie kiuno mwenzio mpaka ukirudi nyumbani cha kwanza ni kufua gwaguro au kificha faragha, kutokana na kuingia madoa yatokanayo na unyevunyevu uhusianao na sehemu za kuzalishia watoto.
DUH!
Swali:
- Unafikiri kwanini mcheza sindimba maarufu ni yule akatikaye kiuno sana na Morani wakimasai ajulikanaye kama dansa mzuri ni anayeruka juu zaidi!
- Wewe unajua kucheza muziki?
- Kucheza mziki maana yake ni nini?
Binadamu kiboko kwa kujitafutia madoido ya kuongeza chachandu katika ladha ya maisha aishiyo. Ladha ya muziki ni kama ladha ya chakula ! Muziki uupendao waweza kutomfikisha mwingine kule kunako.
Katika utamu wa muziki, wengine hawakawii kuanza kulia kutokana na muziki kuwahuzunisha.
Swali:
- Ushawahi kuona mtu anacheza mziki huku analia?
DUH!
Usitishike nawaza tu!
SIKU NJEMA!
Nakuacha na MATTAFIX wakikupa LIVING DARFUR
3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
kaka majukumu yamenitinga nakosa muda kabisa lakini huwa napita apa kwa kasi!
tupo pamoja nashukuru kwakunijulia hali
Leo umenikumbusha swali ambalo miaka kadhaa iliyopita,gwiji la muziki huko nyumbani Ramadhani Mtoro Ongora ali maarufu Dr Remmy Ongerea aliwahi kuuliza kwenye moja ya tungo zake..
Muziki ni wa naniiiii eeeeheeee...
Muziki asilii yakeee wapii eeehee...
Muziki hauna mwenyewe ee...
Hivyo kaka muziki auna mwenyewe makanisani,club hata kitandani mziki upo tu...
Nafikiri wengine wanalia pale muziki unapokuwa mtamu mfano wakati wakuonyesha ushirikina wa watu wawili...
eeen kazi njema...au wengine naona uko ufini wakipewa mustamakala kwasababu inamuziki mnene basi wanakuwa wanalia...
mmmh kwaheri
@Chemsha Bongo:Tuko Pamoja!
@Edwin: Kweli uliyosema Mkuu.
Post a Comment