Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

BAHATI na BARAKA zijazo kwa kukosa AKILI!

>> Tuesday, October 09, 2007

Kuwa na akili ni usumbufu mtupu!

Kama ujinga ni sawasawa na kutokuwa na akili, basi.......:

  • Ujinga unastarehe zake ,...
.... kwa mfano starehe kubwa yakutosumbuliwa na kufikiria maswala yaumizayo akili.

Kufikiria mambo muhimu ni noma sana!
Hukawii kuanza kujaribu kutatua matatizo hata yale usiyojua hata pakuanzia.

  • Uzuri wa kuwa mjinga , ...
.....ni pale unapoweza kuuhisi na kuufurahia utamu kisawasawa, kama tu wenye akili wanogewavyo pale watulizapo akili na kuziruhusu hisia zao kuonja utamu.

Swali:
  1. Nani kasema kuwa mwenye akili lazima afaulu mitihani?
  2. Hivi UJINGA ni kukosa akili?


  • Ujinga wa mwenye akili,....
.... ni pale atumiapo akili kufikia kujilamba, kitu ambacho mwerevu mjinga, bila kufikiria wala nini, anauwezo wakustukia lawalawa ,hata kama mwenye akili anadai kabahatisha, na kumumunya utamu mpaka kisogoni.

POLENI sana WADAU, kwa kuwa na akili!

SASA MTAFANYAJE?


DUH!

Naacha!

Siku njema!

Lakini ngojea LINTON KWESI JOHNSON , atukumbushe yaliyomkuta alipofika UINGEREZA.

Basi bwana endelea tu na Linton KWESI

5 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 11:04 am  

Ujinga jambo lakujichagulia...mwerevu mjinga...duh? Maisha raha kweli:)

Simon Kitururu 1:44 pm  

@Serina: :-)

KKMie 3:30 pm  

Ujinga nadhani sio kutokuwa na akili bali ni kutokuwa mwelevu na huna ule uwezo wa kukumbuka vitu ambavyo unajuwa wazi havikusaidii au havitakusaidia kwa wakti huo.

Vilevile inawezekana kabisa kuwa ujinga ni uzembe au uvivu wa akili yako.

Hivi kwani akili ndio ubongo?

Kuwa na akili sio lazima ufaulu mitihani mimi nina akili na sikuzote ni mtu wa kufeli tu (i mean mitihani) ila ukiniambia nikuelezee jambo kwa ku-type au kuongea unaweza kunikimbia au kuniogopa na kusema "Dinah anaakili sana".

Kwa tafasiri yangu binafsi nafikiri akili ni ujanja wa mtu:-)

Simon Kitururu 4:33 pm  

@Dinah:Akili si ubongo, ingawa bila ubongo huwezi kuwa na akili:-)

Nakubali kuwa kuwa na akili na hata tafsiri ya nani ndio anaakili inaweza ikawa ni janja tu za watu.

Tatizo nikugundua nani mjanja. Maana janja nyingine mtu ajisifiayo inaweza ikawa sio janja bali ni kujikomesha mwenyewe.

luihamu 5:39 pm  

Hakuna ujinga,naamini hakuna mtu mjinga,naomba kuuliza swali,Katibu Mzee Simon yule bwana alibuni lile bomu lililouwa watu kule HIROSHIMA NA NAGASAKI ni mjinga au mwerevu?sasa basi mgunduzi wa AK47 ni mjinga au mwerevu?na ya IRAK BAADA YA KUVAMIWA NA MAJESHI YA MAREKANI TUTAITA NINI?

Rasta anaamini kabisa hakuna ujinga au mjinga ni swala la mazingira.

SIFA NA UTUKUFU KWA MFALME HAILE SELLASI I.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP