Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

MUDA DOMO KAYA! Siri yako yaweza kuwa nje baada ya muda!

>> Thursday, October 11, 2007

Fanya ufanyalo, sema usemalo, baada ya muda fulani ukweli utajulikana.

Kudanganya kwangu leo ni kuzuri.

Tatizo ni kwamba, baada ya muda, unaweza ukastukia hako kakitu nilikokudanganya sikapendi kuwa kananinogea.

Mimi naaamini kuwa, kitu chochote usicho na uhakika nacho , baada ya muda fulani utahakikishiwa,

Samahani!
......Hili swala linagusa mpaka maswala ya kama kuna Mbinguni au hakuna.

DUH!

Ukiwa huna uhakika, subiri , muda utakuhakikishia kuwa:

  • Jamaa hajali
  • Mbinguni na Jehanamu kweli kupo
  • Kweli Yesu ni Mwana wa MUNGU
  • Kuwa jamaa mjinga
  • Nanihino alidanganya

  • Kweli anakupenda.

  • Jamaa Mwerevu
  • Na kadhalika kadhaa...



Tatizo la kusubiri muda, ni kwamba ; kusubiri hakuna mpango!
Kusubiri kunaboa!

Tatizo jingine ni kwamba, muda hausubiri, unakwenda tu.

Leo yule dogo aliyekuwa anakusalimia kwa heshima wakati fulani, anaweza akawa anakuangalia kwa jicho la kukutaka. Inamaana tayari anajilinganisha kinamna na wewe, au sehemu zako fulani za faragha ashajua kuwa anaweza kuzihimili.Hapo ujue muda ndio umeanza hivyo! Si unakumbuka ulipoanza kupewa shikamoo, au mawazo yako kuhitajika kimchezo mchezo tu?

DUH!

Swali fulani:
  • Hivi muda unakwenda wapi?

Lakini....

Binadamu wengi hujenga ukweli wa mambo kichwani mwao, hata kama jina halisi la ukweli wao huo ni uongo. Watu wa namna hii , hata uwape muda, watautumia kutafuka jinsi ya kuhalalisha kaukweli wakaaminiko kuwa ni ukweli.

Wakati wakikuambia wanajaribu kutafuta ukweli wa jambo, huwa wanajaribu kutafuta vigezo vya kujihakikishia kuwa wanachoamini tayari akilini mwao kuwa ndio ukweli.

Hivyo ndani ya ka-Muda fulani...
  • Wakristo, Waislamu, Wabwiti, Wachawi,nk; wanapata vigezo kuwa wanafuata dini ya ukweli.
  • Walevi , watumia madawaya kulevya, walafi, nk; wanapata vigezo kuwa , hawadhuriki.
  • Wanafunzi , wanajisikia kuwa wanaakili baada ya kustukia kirahisi jambo waliloambiwa gumu.
  • Hausigeli na Hausiboi wanawezakujisikia nyumbani, katika nyumba ya bosi wao, na ikawa ni ukweli kwao, mpaka watakapostukia mshahara unachelewa.

  • Wakereketwa fulani hustukia kuwa wanaweza kuibadili dunia , na kuifanya iwe nzuri zaidi.
  • wa......wana....

DUH!

Ngojea nikupe MUDA ili ugundue kama nilichoandika ni upumbavu au sio!

DUH!


Naacha hili swala basi!

-----------------------------------------------------------
Ngojea basi nikutembeze katika mabadiliko yangu binafsi ,
....katika kona, kwa kutumia picha, wakati nikiendelea kuwajibu wadau kadhaa wanaoniuliza sana maswali fulani kwa muda sasa hivi.



SAMAHANI KWA Quality mbovu kidogo za picha ambazo nimeziscan midamida ili, kunisaidia kukusimulia hadithi inihusuyo kama nilivyoathiriwa na MUDA.

Kabla sijaanza , Unamkumbuka MAXI PRIEST?



Tuanze basi........


Hadithi Hadithi!

Simon enzi hizo......



Maisha yalikuwa matamu. Ukitaka kitu unakililia. Chakula kikichelewa unalalamika .Hujui kuwa wazazi wanatoa wapi pesa wala thamani ya pesa nini, wakati unauhakika wa kupata pipi gololi.


Muda Ukaenda wee, ukaenda weee...
Nikajikuta niko Sekondari /A-levo, nikisumbuliwa na matatizo mengine tofauti yaliyojitokeza....
....

Ni vigumu kuyataja yote, mpaka ya chakula kibaya shuleni. Ila kipindi hiki nakikumbuka sana kwa jinsi nilivyomtafuta Mungu , kitu ambacho bado naendelea kufanya. Mpaka kufikia kipindi hiki , nilifanikiwa, kuokoka, Baada ya kupata msaada wa Moses Kulola, Kuslim, baada yakukutana na mafundisho ya Korani, na kuwa Rasta. Mpaka sasa hivi ukinisoma hapa MAWAZONI , utastukia kuwa bado nafuatilia sana maswala ya dini maswala ya dini , nakujiuliza sana kuhusu Mungu , Shetani na .....

Lakini....

Katika kipindi hiki nilifanikiwa pia kupigwa buti na mwanadada niliyempenda.Na ndio ilikuwa mwanzo wa kustukia ugumu wa kuwa na mpenzi mbali nawe , hasa kutokana na kuwa mwanafunzi wa bweni, katika shule ya Wavulana watupu.

Tulikuwa tunatembelewa na akina dada wa MSALATO lakini, kama...


Duh!
....Sijui mdau wangu Godwin Mabagala ambaye tulikuwa tunashea chumba Mazengo na Mdau Kusirie ,wako wapi siku hizi.


Ngojea nikutonye kidogo kuhusu enzi zangu za URASTA...
DUH!
Sijui JAH Kimbuteh na Ras Pompidou wako wapi siku hizi....


Nachojaribu kusema....
.....nafikiri tungekutana na Rasta Luihamu enzi hizo, tusingekuwa tunabishana sana mitazamo, ingawa nakiri kuwa mimi ni mgumu kuaminishwa kitu ambacho akili yangu inashindwa kukubaliana na majibu kinipayo.

Nasikitika kukiri kuwa, nimejiuliza maswali mengi sana, wakati niko ndani ya dini zote nilizowahi kuwepo ndani yake , huku nikipima majibu dini hizi zinipayo, na kujiuliza tena zaidi kama majibu haya yananifikisha katika mridhiko au la.
Nasikitika tena kukiri, mara nyingi nimefikia kuaambiwa, dini haihitaji utumie sana akili kufikiria majibu upatayo ndani yake, la sivyo ,utajikuta huna dini.

Lakini.....

Katika Ukristo, niliweza kuwa bingwa wa mahudhuriao mazuri, muimba kwaya, na hata mcheza maigizo ya kanisani , kama hapa nionekanavyo, ndani ya kanisa la BUNGO , MOROGORO...





DUh!

Kuna kitu kingine wadau fulani hupenda kuuniuliza sana .
Hasa swala lakutochana nywele .

Kwanza napenda kukumbushia kuwa mimi kiimani sio RASTA kama wengi waaminivyo kuwa ukiwa na nywele kama zangu , basi wewe ni RASTA.

Pili , naamini unaweza kuwa na nywele za staili yeyote ,ingawa kumbuka kuwa dunia imejaa watu wepesi kuweka watu katika mafungu. Kwahiyo unaweza kukosa kazi sehemu kwa sababu tu unavaa lubega na sio jeans.

Mimi mwenyewe, mpaka leo hii, ukikutana na Baba yangu, ingawa ni mtu mwenye diplomasia, kama umesuka au Huchani nywele kama mimi, ujue kabisa kuwa atakuwa na mashaka nawe.

Dingi yangu anaamini , kijana nadhifu na waheshima, ni lazima atakuwa amekata nywele vizuri. Hawezi kukuelewa , kama wewe ni mwanaume halafu umesuka nywele. hawezi kukuelewa , kama huchani nywele kama mimi.

Kwa bahati mbaya, mimi nimepitia katika vyote vitatu. Kukata nywele, kusuka, na kuwa na locks kama nilivyo hivi sasa.
Unaweza ukastukia mionekano yangu kadhaa tofauti na mpaka mdingi wangu katika picha hizi...


Vilevile...
kuna jamaa wengi huniuliza kama mimi ni msanii au la!
Naweza kukiri kuwa mimi ni mpenzi wa sanaa. Nimefanya sana miaka kibao , ingawa sijasomea hii kitu wala sijawahi kujiita Msanii. Nimefuata sana mdundiko, kuigiza mpaka vijijini, na pia kupanda majukwaa kibao tu.
Baadhi ya viwanja enzi hizo....

Lakini...
Mimi , tokea nianze kuuza magari ya waya na ya makopo SONGEA, halafu nihamie kwenye uchumi , kimasomo High School, na Biashara kabisaaa, katika vyuo kadhaa., nakiri kuwa mimi ni MFANYABIASHARA.Usistuke kustukia siandiki maswala ya biashara humu.

USITISHIKE na NYWELE!

........Mwisho wa hadithi!

Naamini kuna baadhi ya wadau, mliokuwa mnanilenga mara kenda fulani na maswali fulani, nimewajibu kiasi.

MUDA UTAJIBU MAMBO MENGINE!
AU?



TUKO PAMOJA!
Samahani nawarudia KASSAV wakija na kitu SAMMI

6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

luihamu 6:19 pm  

Mzee Katibu Simon kama Mfalme Sellasi alivyonena ni lazima kuheshimu imani ya binadamu yeyote yule.

Mzee Simon,JAH anakupenda sana na najuwa unajuwa JAH anakupenda.

Lakini huko kote ulikuwa unatafuta nini?ULOKOLE,UISLAMU NA URASTA?
Je tuseme ulikuwa haujiamini?kuna mtu au watu walikuwa wanakuogopesha?

Ngoja kwanza...kwa hiyo wakati ule uliweza kukemea na kunena kwa lugha?

Katibu naheshimu imani yako napia nakuheshimu sana.

Simon Kitururu 1:36 am  

@Rasta Luihamu:
Nilivyookoka,ku......, sikufanikiwa kunena kwa lugha.:-(

Katika kupitia dini kadhaa, ilikuwa sio kutojiamini. Nahisi kujiamini ndio kuliniponza mpaka nikaanza kutafuta majibu sehemu sehemu nyingine na kuhamahama.
Si unajua maisha ni shule? Ndio maana mpaka leo sina jibu kamilifu . Nikipata jibu, utasikia nimeanzisha dini.

SITANIII!


Naheshimu dini zote. Na naheshimu watu wote. Ukiona nimemkosea mtu heshima , ni kutokana tu na ubinadamu wangu, lakini kama unanijua ,utaamini kuwa mimi nina heshima kwa kila mtu.

Ninatatizo la kujiamini sana, ndio liniondolealo ulaji mara nyingine.

Si , unajua ulaji mwingine ni lazima uitikie tu na kujifanya huelewi?

Najifunza lakini kucheza ``Play fool fe catch wise´´

KKMie 4:05 pm  

Dah! Umenichekesha sana nilipofika kwenye Jah Kimbute na Ras pompidu (hivi huyu ndio alikuwa nani vile? hili jina nilikuwa niliksikia wakati ule naanza shule).

Picha ni kumbu kumbu nzuri sana, asante kwa ku-share na sisi......inaelekea wewe ni mdadisi sana...Ulokole, Uislamu, Ujah na sasa uko wapi?

All the best best :-)

Simon Kitururu 2:35 am  

@Dinah: Jah Kimbuteh alikuwa ndio mpiga muziki wa aina ya Reggae maarufu enzi hizo Tanzania. Ras Pompidou alikuwa naye mwanamziki wa miondoko ya Reggae na mingineyo pia. Mara ya mwisho nilisikia Ras Pompidou alikuwa na Bendi ya INAFRIKA hapo DAR, ila wote wawili sijui wako wapi.

Siku hizi bado naamini MUNGU! Ila ni mwoga wa imani zozote zenye institutions

Egidio Ndabagoye 8:40 pm  

Dah! mambo ya imani magumu sana.Kwa kifupi dini naziita kama chama cha siasa,kesho unaweza kuwa TLP keshokutwa CUF lakini dhumuni ni lile lile.

Macca pia nilipitia lakini sikujikita sana na niliingia kule kwa sababu fulani ili nipate kitu fulani.
Si unajua mzee unaweza shawishika kuingia kundini kumbe unahitaji maslahi fulani.Mambo haya tena....

Nipo Mbioni kulazimishwa kuingia dini ya Hindu!

Mwanzoni nilipoanza kujiuliza sana masuala haya ya dini ilifikia nikaacha kwenda kanisani.Lakini baadae nikanza kwenda tena lakini nikaacha kutoa sadaka.

Mapicha yametulia mkuu yanatoa somo fulani

Pius Ntwale 1:09 pm  

Wakuu nami nichangie patamu hapa, Simon kumbukumbu bomba sana umeweka!
Nianze kwa kusema kuwa ninakiamini kila kilichoandikwa ndani ya biblia!
Ni ugumu wa kuamini ndio uliomfanya Mungu amwambie Musa ishara zitafuatana naye ili Farao awaachie wana wa Israel,lakini bado Moyo wake ulikuwa mgumu, mkisoma maandiko kama yalivyoandikwa katika kitabu cha kutoka mtaona,someni!! sishangai mki 'doubt' kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu!
Ni kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya binadamu ndio maana Bwana Yesu alitenda miujiza kibao ili watu wamuamini,wapo walioamini na wapo waliokataa kumuamini wakaamua kumsulubisha!
Swali ni je mnakiamini kilichoandikwa kilichoandikwa katika maandiko?, ninaongelea biblia, ndiyo niisomayo!
Hivi mngalikuwapo enzi hizo mkamuona yule kipofu aliyefunguliwa macho na Bwana Yesu bado mngeliendelea kuelea katika imani au mngeamua kuzama?
Manake binadamu huhitaji kuona kwanza ili ajishawishi kuamini!
Anyway binadamu tu dhaifu na mara nyingine tunatetea kaudhaifu ketu kwa ajili ya kuendeleza yale ambayo kama tungaliamini tusingaliweza kuyaendeleza!!!!!!!!

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP