Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUSEMA, KUZUNGUMZIA ,KUTENDA kwa VITENDO, vyote VIMEDUMAA!

>> Wednesday, October 03, 2007

  • Kusema, kuzungumzia, hata kutenda , vyote vina asilimia fulani za kucheza pata potea.

Ukiandika.......

.... inawezekana unatumia maneno mengi bure, kufikisha ujumbe usiofika.

Ukisema......

...inawezekana unatumia sentensi zako na nguvu zako bure, kujaribu kufikisha ujumbe ambao ungefanikiwa kutofika kwa sentensi au maneno machache tu na bila mabavu.

Swali:
  • Nani kasema ukifanya kwa vitendo , vitendo vyako vinafikisha ujumbe kwa wale wahusika uwalengao?
  • Unafikiri kitendo cha Mwalimu Nyerere kujilimia kwa jembe la mkono kilifikisha ujumbe gani kwa akina KIKWETE?
  • Unawakumbuka, Yesu , Mitume, Manabii kibao, wa dini kibao walivyofanya kwa vitendo , halafu siye na nyie mpaka leo tunafanyiakazi kujua walikuwa wanatuambia nini?


SEMA, ZUNGUMZA,au TENDA kivyako.
INAWEZEKANA unajifikishia ujumbe wewe mwenyewe.

INAWEZEKANA WEWE MWENYEWE NDIO MUHUSIKA KATIKA UJUMBE ujaribuo kuwafikishia wengine.


TENDA WEMA UENDEZAKO, usisubiri kitumbua.

DUH!

Swali:
  • Leo umeshafanikiwa kutofikisha ujumbe?
  • Hivi inawezekena kujifikishia mwenyewe ujumbe?

Nakuacha na Barry White

1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Anonymous 1:13 am  
This comment has been removed by a blog administrator.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP