Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

KUHUSU MTAZAMO WAKO KATIKA SWALA!

>> Monday, October 29, 2007

Nikisema, utanikatalia!
Kisa, mtazamo wako na wangu vinatofautiana.

Katika mtazamo, king'ang'anizi anawezakuonekana kashinda, ingawa ashindwaye hoja bado inawezekana kashinda kimtazamo wa tikitaka.

Katika mtazamo mmoja Papa ni baba mtakatifu ,wakati mwingine unafikiria nje ya mtazamo, kama, hivi watakatifu wasio na wake au wanaume wanatibuje hamu takatifu za kibinadamu za uroda?

DUH!

  • Nakubali kabisa kwa mtazamo fulani Afrika ni maskini na kuna magonjwa kibao kama tuonavyo kwenye televisheni fulani.

  • Nakubali kwa mtazamo fulani inabidi niache hata kufikiria swala hili la mtazamo.

Swali:
  • Kwa mtazamo wako unafikiri mtazamo wa mwenzio ni bomba kuliko wako?
  • Kwa mtazamo wako, hivi ni nani anaenda mbinguni vile?

Duh!

Kwa mtazamo wangu ngojea niachie hapa hapa, kabla mtazamo wako haujaanza kufikiria kwanini naandika kuhusu swala la mtazamo ambalo inawezekana kama umesoma mpaka mstari huu , ukawa umejipotezea muda wako bure kwa mtazamo fulani.

DUH!
Nimtazamo tu ndugu yangu !
AU?
Tulia na Bendi ya Kisauzi SOUL BROTHERS

3 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

Said Michael 7:23 pm  

Japo kila muwamba ngozi huvutia kwake! lakini kuna wakati inabidi mtu ukubali kuwa mtazamo wa mwenzako ni BOMBA zaidi ya wako kutokana na jinsi alivyo Tazama Mbali Zaidi (TAMBAZA).

Kuhusu swala la nani atakwenda Mbinguni; Hii ni sawa na siri sirini.

MADA ZAKO MKUU ZINAFANYA NIWEZE KUFIKIRI MBALI ZAIDI YA NINAPOFIKIRI.

Kanyaga twende, tupo pamoja

Mijadala 7:58 pm  
This comment has been removed by the author.
Simon Kitururu 8:00 pm  

@Said:Umenimaliza na TAMBAZA hapo mkuu!
Kweli kabisa mara nyingi tu unaweza ukastukia jicho la mwenzio limestukia ambacho hukukistukia. Ila wengi wetu ni wagumu kukiri kuwa mwingine kapatia mtazamo wa swala, ikiwa mtu anakubali kuwa kuna kitu kama mtazamo potofu.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP