KWA MPENDWA MWANANGU MSENGE!
>> Saturday, October 27, 2007
Swali:
- Ngono kwako ni kiburudisho au unataka kutengeneza mtoto?
- Hivi wasenge na Wasagaji wana kasoro?
Pamoja na kufurahia na kuguna kwa utamu wa kuzalisha, (hasa ikiwa sio wewe uko leba wodi) wengi tunabunia tu, na kujihakikishia mtoto aliye mimbishwa atakuwa kama tumnuiavyo
Atakuwa.....
- Bomba..
- Ana akili huyo!We acha tu!
- Daktari hapo baadaye
- mwanaume au mwanamke.., (kama ni mwanaume ,hakawii kukuletea kesi homu za kumimbisha kuanzia hausigeli mpaka mtoto wa padri , halafu humaindi sana!).....
- Anacheza sana basketi boli
- ......... nk kadhaa zisababishazo unamtambulisha kila chobisi......nk.
Kwa ujumla , mwenye mtoto hawezi kunuia kirahisi toto lake liwe na kasoro fulani.
Mtu unajikuta tu umezaa mtoto kilema au yuko dakika kadhaa nyuma katika idara ya kufikiria.
Huwezi kuwa umechagua kirahisi kutengeneza toto usilojivunia.
Ingawa wengi wakati tunacheza kamchezo, hatukumbuki kuwa ni kamchezo kawezako kumimbisha mtu.(hapa ni kama wewe sio basha ahusuduo saresare maua au yule.....ndani ya kale kamchezomchezo)
DUH!
Ukiachana na mengine mengi ambayo yatajitokeza katika mtoto wako yakusikitishayo, hasa kutokana na tabia za binadamu kujenga mategemeo ya kutegemea toto lako litakuwaje au litafanya nini hapo baadaye....,naamini kuna mengi ya kushukuru tu kuwa, angalau umefanikiwa kulipata toto lako.
Sasa ukishalipata toto lako zuri na lina akili hilo, na halisahau kukuletea mlenda na kale kagari fulani liliko kununulia na kuhakikisha unapata mafuta na.....
DUH!
Naacha Basi!
Mcheki kidogo Harry Enfield akichekesha katika kugusia swala la mtoto wa kiume akimleta bwana wake wakiume nyumbani...
Swali:
- Utafanyaje mtoto wako mpenzi akikustua kuwa anahusudu nanihii za faragha zifananazo na zake?( namaanisha, akiPENDA SARESARE MAUA?)
Sina mtoto bado!
Inawezekana nawazia jambo nisilolijua!
Naaacha basi!
Tulia na Los Lonely Boys wakikupa kibao MBINGUNI
2 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Wote wangeimba hivi kanisani bila shaka ningekuwa regular huko. Kuhusu mambo unayoyazungumuzia na watoto ...kuna ile picha wazazi wote wanao lakini ukweli nao ni kitu kingine. Sio tu mtotot akwa mchanga...hata akisha baleghe na kuwa mtu mzima...maswala kama...mwanangu hajao,mwanangu hana watoto, mwanagu amekuwa amekimbilia madawa, mwanangu siku hizi haji kututembelea sisi wazazi wake....nk. Matarajio huwa ni mengi na tusipotimiza matarajio ndipo sifa zapotelea huko! Lakini kama mzazi...unapotazama furaha mwanao anayokuletea kwa njia zingine, yale madoa hutayaona...sio kuwa mwanao hana kosa ila umeamua kushangilia mazuri...mambo ungependelea kukumbuka....ndio hali ya binadamu.
@Serina!Nakubaliana kabisa na wewe.
Ngojea na mii nitafute wa kutengeneza naye mtoto ili niingie ndani ya swala nililokuwanaliwazia:-)
DUH!
Post a Comment