USHAWAHI KUNYIMWA?
>> Saturday, October 13, 2007
- Mkubwa , ukinyimwa kitu baada ya kukiomba, unakifanyia kazi. Ukikifanyia kazi , lazima ukipate kama kilekile ulichonyimwa,hapo ni kama imeshindikana kupata ulichonyimwa.
Ukizaliwa tu, unaanza kunyimwa kitu fulani.
Unanyimwa hata chuchu, kwa faida yako mara nyingine.
Ukiwa unakua lazima ukutanane sana na sentensi kama; ``WEE ACHA ! au, Nani kakupa pipi, utaoza meno wewe, hebu tema hiyo lawalawa sasa hivi!´´
Lakini....
Ukiwa mdogo , baada ya kunyimwa chuchu, unaruhusiwa kuililia.
Ukiililia mara nyingine unapewa.
Baada ya kuililia na kunyimwa zaidi unalala.
Lakini.....
Kuna watu wanasema kuwa , ukifanyiwa kitu fulani mara nyingi, utazoea.
Ukweli ni kwamba, kukubaliana na kunyimwa au kuzoea kunyimwa ni vigumu.
Mara nyingi mtu akinyimwa lazima anyong'onyee.
Ukinyimwa unaweza pia ukaanza kuogopa kuomba tena ,kutokana na machungu uyakumbukayo au uliyopata baada ya kunyimwa..
Swali:
- Unahisi unaweza kunyimwa kuingia mbinguni pamoja na kuomba kwako huku?
- Ushawahi kunyimwa salamu na uliyehisi angekusalimia?
- Ushawahi kunyimwa............na ..................?
USITISHIKE!
Kunyimwa ni kawaida!
Kunyimwa inaweza ikawa ni changamoto kwako, ambayo itakupeleka mbele na sio kukudumaza.
NAKUTAKIA WIKIENDI njema NA kila la kheri katika KUGEUZA machungu ya kunyimwa, YAZAE MATUNDA yatakayo msababisha AKUNYIMAYE akuombe urafiki!
Nakuacha na nyimbo mbili kutoka kwa SOLOMON BURKE na 2Face Idibia ,zikusindikize kwa muda wa siku kadhaa ambao sitakuwa mtandaoni kwa sana!
Solomon Burke...
2Face IDIBIA
TUKO PAMOJA!
6 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
bwana KITURURU usiombe kunyimwa,ni balaa!umenikumbusha nikiwa mtoto nambiwa nilikua mbishi balaa hasa ninapohitaji nyonyo alafu nikanyimwa,lakn hapa mkubwa nataka nitofautishe kunyimwa kwa utoto na ukubwani kwani kimsingi ukinyimwa ukubwani hasa need inapokua ime arise unaweza uwa mtu,pia kuna mambo ambayo yanamvuto wa kijamii hasa kimw...katika kutekeleza siri ya uumbaji uwa kiu yake haikatiki kwa maneno matamu hata kamayawe kama lawalawa ni lazima upewe unachokiitaji.nice uchambuzi kaka
Kaka nakusalimu kwa jina la JAH.
Tume kumbwa na msiba mkubwa sana jumuiya nzima ya wapenda Amani na usawa.
Hatimaye hatunaye tena Luck Dube.
Pumzika kwa amani Dube
Simon,
Hii falsafa ni nzito,pana na ndefu.Nadhani kwa juu unaongelea kunyimwa.Lakini ndani mwake kunawezekana kukawa na falsafa.Ona sasa,ushaninyima usingizi wangu na badala yake inabidi niketi nichambue unaongelea nini hasa.
Ebwanaeee...! Kunyimwa si mchezo inauma moyoni! Lakini kumnyima mtu kitu usichopenda kumpa nayo vipi raha au?
@Jeff na Said:Kazi kwelikweli!
@Ndaki:
Kweli bomba la msiba hili!:-(
Tuko Pamoja Kaka!
Post a Comment