Mtakatifu SIMON KITURURU - MAWAZONI

FALSAFA na WAZO ndani ya neno - DUH!

Katika Kuchagua Nani wa Kumuua.

>> Friday, October 26, 2007

Kuua ni dhambi kwa wengine.
Kuua pia wengine huita adhabu au njia ya kuabudu.

Kuua ni rahisi hasa kwa binadamu aliyefanikiwa kujidanganya kuwa kitendo chake cha kuua si kuua.

Swali:

  • Ushawahi kupiga au kutamani kupiga mwizi?(Si unakumbuka ngumi moja yaweza kuua?)

  • Ushawahi kula nyama au samaki?


Staili ya kuua ni madoido tu.
Unaweza kuua kwa kutomjulia hali mtu.

Katika ajali....
......unaweza ukajikuta unachagua nani wakumuokoa kwanza.
Wakati unachagua wa kumuokoa kwanza, inawezekana umechagua nani afe

Usitishike!

Binadamu ni mtu mzuri, mara nyingi huchagua kufa yeye mwenyewe .
Hakawii kucheza peku kiwanja chenye miba!
Akiwanazo hakawii kula mpaka augue.

DUH!

Wiki mwisho Njema! Wadau!
Nakuacha na kaka Freddy Macha

8 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:

KKMie 9:05 pm  

Hii imenigusa sana kunako moyo lakini in a way inafanya mtu ujione muuwaji au umeshawahi kuua kwa kuchinja mnyama ili upate nyama, vilevile kuchagua nani wa kumuokoa bila wewe kutambua kuwa unachagua.

Kwa wajinga-wajinga itawasaidia kuona kuwa kuuwa ni kitu cha kawaida kwani sote tumewahi ama tunaua kila siku in a way bila kujijua.

Unajua unapouwa panya, mendem unamkanyaga sungusungu au sisi mizi.....mbu akikung'ata unamtandika kibao na anakufa mwilini mwako.....huko ni kuua sio?

Maneno mazuri ila nimetishika kiaina.

Simon Kitururu 12:08 pm  

@Dinah!
Kuna mambo mengine ukiyafikiria , lazima utishike!
Kazi kweli kweli!

Anonymous 1:13 pm  

Nimependa jinsi umemchagua freddy hasa kufuata ujumbe ulioandika hapo juu...who brought disorder to africa anauliza...twauana wenyewe kwa wenyewe...Duh! nami wacha niingie mawazoni.

Simon Kitururu 2:21 pm  

@Serina:Kazi kwelikweli!

Anonymous 11:16 pm  
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous 11:10 am  
This comment has been removed by a blog administrator.
Anonymous 5:26 am  
This comment has been removed by a blog administrator.
Affordable Luxurious Wedding Dress Blog 4:33 am  
This comment has been removed by a blog administrator.

Idumu Jumuiya Ya Wanablogu Tanzania


Photo Sharing and Video Hosting at Photobucket

Partner

save mt. Kenya campaign
In partnership with africapoint.com

Taswira BANANGENGE

  © Blogger templates Romantico by Ourblogtemplates.com 2008

Back to TOP