BAADA ya kumsikiliza na kuangalia kazi zake GURU wa YOGA, B.K.S. LYENGAR.......
>> Thursday, October 04, 2007
Baada ya kufuatilia kazi za GURU LYENGAR , sikuacha kujiuliza; ni kazi ngapi za Kiafrika ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ili kueleweka au kufundishika kirahisi?
Huyu Guru, alifanikiwa kuchukua tamaduni ya YOGA na kuipanga kinamna ambayo watu wengi wanaweza kuielewa na kujifunza. Na uhakika kuwa kuna watu wengi wenye taaluma za asili za Afrika, ambao wangeweza kuzijenga kinamna ambayo tunaweza wote kuelewa kirahisi, zinafanyikaje.
Swali:
Hivi kwa nini taaluma ya Uchawi Afrika, tunafundishana kinyemela?
Hivi nani anafuatilia na kuturahisishia uchezaji wa sindimba?
DUH!
Tukiachana na Guru kidogo....
Nimefurahi kuona kazi za Bi Kidude na historia yake.
Naombea sisi wote, pamoja na wasanii waliokubuhu na wajuzi wa mambo yetu yafanyayo tutambulike kama Waafrika , wote kwa pamoja tuendelee kufanyia kazi za kuhifadhi na kuendeleza tamaduni zetu.
Hebu tumcheki GURU B.K.S LYENGAR
Mwaka 1938 akifanya vitu vyake...
Mwaka 1991 akiendeleza...
Akiongea...
Tumalizie kidogo na BI KIDUDE ,ambaye anaenda MIAKA MIA MOJA na hajaacha fani, aendeleze!(Ukitaka kumjua zaidi tafuta kazi imuhusuyo iitwayo AS OLD AS MY TONGUE)
1 KOMENTI a.k.a Maoni. :-(:
Post a Comment